Mkurugenzi wa Mkwawa trail run, Amani Mkwawa akiwa na
Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Hamid Njovu wakiongea na waandishi wa habari juu ya mashindano ya mbio za Mkwawa jinsi gani zitakavyo fanyika hapo baadae
Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya Iringa Hamid Njovu wakiongea na waandishi wa habari juu ya mashindano ya mbio za Mkwawa jinsi gani zitakavyo fanyika hapo baadae
Mkurugenzi wa Mkwawa trail run, Amani Mkwawa akiwa na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoani Iringa walioshiriki mkutano wa kutangaza kwa kuanza kwa mashindano ya Mkwawa Trail Run
NA
FREDY MGUNDA,IRINGA.
MASHINDANO ya Mbio za Mkwawa trail run yatafanyika
Iringa Juni 16 mwaka huu kwa lengo la kutangaza utalii wa nyanda za juu kusini.
Akizungumza
na blog hii mkurugenzi wa Mkwawa trail run, Amani Mkwawa alisema kuwa wanariadha
watakaoshiriki mbio hizo watakimbia katika mazingira ya mabonde milima na kuvuka
mito huku washiriki wakipata historia ya eneo katika kila kituo.
“Mbio
hizi ni tofauti na mbio nyingine, hizi zitapita katika maeneo yote yaliyotumika
na Chief Mkwawa wakati wa mapambano dhidi ya Ujerumani huku zikirindima
kupitia kwenye mabonde, milima, na vivutio vya kihistoria,” alisema Mkwawa.
Mkwawa
alisema kuwa mashindano yatafanyika mkoani hapo kwa lengo la kuchochea shughuli
za kiuchumi kwa kutangaza fursa za uwekezaji biashara na vivutio vya kitalii
vilivyopo Iringa na nyanda za juu kusini.
Kutunza
mazingira na kuendelea kukumbuka na kusherekea maisha ya mashujaa wetu
mbalimbali waliotangulia katika kupigania taifa.
Mkwawa
alisema kutakuwa na zawadi mbalimbali katika kumbukumbu hiyo kama medali, vyeti
na fedha taslimu kwa washindi watatu wa mwanzo.
Kwa upande
wake Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata aliwaomba wananchi wa mkoa
wa Iringa na nje ya Iringa kushiriki katika mbio hizo ili kukuza utalii wa
nyanda za juu kusini.
“Hizi
mbio zitasaidia kukuza uchumi wetu kwa kutangaza vivutio vilivyopo hapa mkoani
Iringa ambavyo hapo baadae tutapa watalii wengi ambao watatuongezea kukuza
uchumi wetu” alisema Lyata
Lyata
aliongeza kwa kusema kuwa mashindano haya yanasaidia kuendelea kumkumbuka
shujaa wa mkoa wa Iringa marehemu chief Mkwawa na wananchi kujifunza namna
chief huyo analivyokuwa mchapa kazi.
“Nitoe
rai tu kwa mwananchi yeyeto yule ambaye yupo tayari kushiriki mashindano haya
anakaribishwa kwa kuwa kila kitu kinaendelea vizuri na niwakaribishe kuweka
historia kwenye mbio hizi” alisema Lyata
Naye Naibu
Katibu mkuu wa Iringa Tourism Association, Serafino Lanzi amesema washiriki wa
mbio hizo watakimbia katika njia ambazo Chifu Mkwawa alipita na kuacha historia
ya Mji wa Iringa.
“Mkwawa
Trail Run imeandaa njia kufuatana na historia ya maeneo hayo na mbio zitaanzia
Uwanja wa Mashujaa Kalenga ulitumiwa na Mkwawa watapita njia ya Mkoga kutokea
Kipongoma ambapo ni chimbukizi la mama yake Mkwawa na kupata historia.” Lanzi
Lanzi
alisema kuwa washiriki wa mbio hizo watapita Nzihi kurudi Kalenga njia ile
alipita mama yake Mkwawa wakati anaenda kutupa dawa zake pale pia tutapita
kwenye njia ambayo alitokea Chifu Mkwawa baada ya Wajerumani kupiga ngome
wakati anaondoka kwenye ile njia anatokea na mahali hapo ndipo alimuua
Mjerumani aliyetaka kumpiga picha Mkwawa.
0 comments:
Post a Comment