
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akizindua kiwanda cha maji – Mkwawa kilichopo mjini Iringa, Septemba 25,
2019. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu,Mama Mary
Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Ali Happy, Mkurugenzi Mtendaji wa
Kiwanda, Ahmed Huwel, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel
Nyamahnga, Naibu wa Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege na
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iri ga, Richard Kassera.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimpongeza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha maji – Mkwawa, Ahmed
Huwel baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda
cha maji-Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel kuhusu ujazaji maji katika chupa wakati
alipozindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happy.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maji – Mkwawa, Bw.
Ahmed Huwel kutembelea kiwanda baada ya Waziri Mkuu kuzindua kiwanda
hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
mkewe Mary wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha maji-
Mkwawa, Bw. Ahmed Huwel (wa tatu kulia) kutembelea mitambo ya kuzalisha
maji baada ya kuzindua kiwanda hicho mjini Iringa, Septemba 25, 2019.
Kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, wa
pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Ally Happy na wa pili kulia ni
Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Dkt. Abel Nyamahanga.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua kiwanda cha maji- Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019.

Wananchi wakimsikiliza Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua kiwanda cha
maji – Mkwawa mjini Iringa, Septemba 25, 2019. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment