






………………………
NA.MWANDISHI WETU
Zaidi ya wafanyabiashara na
wawekezaji 390 mkoani Ruvuma wamekutana katika mkutano wa mashauriano
baina ya Serikali na Sekta binafsi ili kusikilizwa na kupata ufumbuzi wa
changamoto wanazokabiliana nazo katika mazingira ya biashara.
Kongamano hilo lililofanyika
Septemba 24, 2019 lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa
kushirikiana na ofisi ya mkoa wa Ruvuma na kufanyika katika Ukumbi wa
mikutano wa Bomba mbili Mkoani Ruvuma .
Kongamano hilo lilihudhuriwa na
Mawaziri kutoka Wizara saba ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano
na Mazingira), Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo,
Wizara ya Nishati na Wizara ya Viwanda
Akizungumza wakati wa kufunga
kongamano hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
masualaya Uwekezaji nchini Mhe.Angellah Kairuki alieleza nia thabiti ya
Serikali katika kuwafikia wawekeza wote nchini kwa kuzingatia maelekezo
ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli aliyoyatoa tarehe 7Juni, 2019
alipokutana na wafanyabiashara Ikulu Jijini Dar es Salaam.
“mikutano ya Mashauriano kati ya
Serikali na sekta Binafsi imejikita kusikiliza na kutatua kero za
wawekezaji na wafanyabiashara katika kada mbalimbali ili kutengeneza
mazingira ya kuwekeza zaidi ili kukuza uchumi wetu kwa ustawi wa
biashara zenu kwa kutambua na kuthamini michango yenu ndani ya jamii na
nchi kwa ujumla,”alieleza Waziri Kairuki.
Alieleza kuwa, mikutano hiyo
ya mashauriano itaendelea kwa nchi nzima ili kuhakikisha mazingira bora
ya wafanyabiasha na wawekezaji nchini kwa lengo la kufikia adhima ya
uchumi wa kati na kuendeea kuwa na nchi yenye maendeleo.
“Mikutano hii inaenda sambamba
na utekelezaji wa Kauli Mbiu aliyoitoa Mheshimiwa Rais kuwa Mwaka 2019
ni Mwaka wa Uwekezaji, hivyo nasi Waheshimiwa Mawaziri tumeamua
kutekeleza hilo kwa Kauli mbiu ya kwamba “Mwaka 2019 ni Mwaka wa
Uwekezaji: Tunasikiliza na Tunatatua”.alisisitiza Waziri Kairuki.
Naye Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji aliwahakikishia wawekezaji kuhusu
maboresho yanayoendelea kufanywa na serekali kwa kuwa na punguzo za
tozo, ada na kodi mbalimbali walizoainisha kuwa ni kero kubwa kwa
wafanyabiashara hao.
“Mhe. Rais alipoingia madarakani
alianza kuboresha viwango vya kodi kwa kuhakikisha anaondoa na kufanya
marekebisho kwa kodi ikiwemo zile za madini, na hii ni dhamira
njema”alieleza Dkt.Kijaji
Aidha alifafanua kuwa, wameendelea
kutekeleza kwa vitendo sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo
imebainisha orodha ya tozo na ada zilizopunguzwa na zilizofutwa na
kuahidi kuendelea kusimamia utekelezaji wa ukusanywaji wa tozo zote
nchini na kushughulikia kero za kodi, ada na tozo zinazotozwa bila
kufuata sheria na taratibu zilizopo.
“Katika Bunge la Bajeti ya mwaka
2018/2019 zaidi ya kodi, tozo na ada mbalimbali zipatazo 109 zilifutwa
na nyingine zipatazo 54 zilifutwa ili kuboresha mazingira ya
wafanyabiashara na wawekezaji,”alisisitiza Dkt. Kijaji
Alimalizia kwa kutoa rai kwa
wananchi kuendelea kufuatilia kila taarifa muhimu zinazohusu maboresho
ya sheria na kanuni mbalimbali zinazohusu ulipaji wa kodi ili kuendana
na mabadiliko mbalimbali yanayojitokeza.
0 comments:
Post a Comment