METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 28, 2017

WATANZANIA WANG’ARA SHINDANO LA MWANDISHI BORA WA SAYANSI NA KILIMO AFRIKA

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano hilo lililofanyika jana nchini Uganda.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ambae alishinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.  
Keki ikikatwa katika hafla hiyo
 
Na Mwandishi Wetu
 
Mwandishi wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ameshinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.
 
Kitabu alikuwa anachuana na waandishi kutoka nchi za Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Shindano hilo lilifanyika jana katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyoko nje kidogo ya jiji la Kampala.
 
Kwa ushindi huo, Kitabu ambaye ni mshindi wa jumla wa shindano la Tanzania, alijinyakulia kitita cha dola za marekani 1,500 pamoja na simu aina ya iPhone 7+ yenye thamani za dola za Marekani 1,200. 
 
Mwandishi mwingine wa Tanzania aliyepata tuzo ni Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye aliwashinda waandishi wengine ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio. ambapo Tanzania ilizidi kung’ara baada ya Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili katika waandishi wa televisheni. 
 
Koleta aliondoka na kitita cha dola za Marekani  1,500, simu aina ya iPhone 7+ ya thamani ya dola za marekani  1,200 wakati  Dino Mgunda alipata zawadi ya dola za marekani  1,000 na simu ya iPhone7+  ya thamani ya dola za marekani 1,000.
 
Katika shindano hilo jumla ya waandishi 20 waliwakilisha nchi hizo. waandishi hao ni wale ambao walikuwa washindi katika shindano la nchi mahalia, shindano ambalo lilifanyika mwanzoni mwa wiki hii katika nchi hizo ikiwemo tanzania. 
 
Shindano hilo liliandaliwa na Jukwaa la wazi la Bioteknolojia za Kilimo (OFAB) ambalo linahamasisha matumizi ya bioteknolojia katika kilimo ili kuwezesha nchi za Afrika ziweze kujitosheleza kwa chakula.
 
 
Mshindi wa jumla katika shindano hilo la jana ni  mtangazaji wa kituo cha  TVC, Omolara Afolayan kutoka Nigeria. Washindi waliteuliwa na jopo la majai watano.
 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com