Mwakilishi
wa Palestina akipokea bendera kutoka kwa Rais wa Interpol Bw. Meng
Hongwei kuashiria uanachama kamili wa Palestina ndani ya Taasisi ya
Polisi ya Kimataifa ya kuzuia uhalifu wa kijinai duniani. …………………………………………………………………..
Mkutano
Mkuu wa Taasisi ya Polisi wa kimataifa wa kuzuia uhalifu wa kijinai
“Interpol”, umekubali kujiunga kwa Palestina katika taasisi hiyo,baada
ya nchi wanachama 75 kulipigia kura ya ndio azimio hilo. Interpol
imethibitisha kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa, Palestina na visiwa
vya Solomon kuanzia sasa ni miongoni mwa wanachama wake.
Interpol
ni taasisi kubwa zaidi ya kipolisi wa kimataifa iliyoasisiwa mwaka
1923, inajumuisha masuala ya nchi wanachama 190,huku makao makuu yake
yakiwa mjini Lyon nchini Ufaransa.Aidha Interpol imekubali uanachama wa
Palestina mnamo siku ya jumatatu iliyopita jioni kufuatia ombi la nchi
hiyo, kabla ya kulijumuisha katika ajenda zake zitakazopigiwa kura
katika Mkutano wake Mkuu,ambao uliketi nchini China Jumatano iliyopita
na kuikubalia Palestina ombi lake hilo.
Kwa
upande mwingine,Israeli na Marekani zilijaribu kukwamisha hatua hiyo ya
kukubaliwa uanachama wa Palestina katika Interpol, kwa kutumia
mashinikizo kadhaa juu ya taasisi hiyo ili isikubali ombi la Palestina
kuwa mwanachama.
Wakati
huo huo, Dr.Riyad Al-Maliki ambae ni Waziri wa Mambo ya Nje wa
Palestina, amepongeza hatua ya kuipigia kura ya ndio nchi yake na
hatimae kukubaliwa uanachama wa Interpol,kupitia mkutano wake mkuu
uliofanyika mjini Beijing nchini China. Amesisitiza kuwa hatua hiyo
inathibitisha kuaminika uwezo wa Palestina katika kutekeleza
sheria,dhamira halisi na maadili muhimu ya Interpol.
Waziri
pia ameashiria kupatikana kwa ushindi huo,kumetokana na msimamo wa
awali wa idadi kubwa ya nchi wanachama wa Interpol, iliyotetea sababu ya
kuwepo kwa taasisi hiyo na kanuni zake za msingi,pale zilipokataa
waziwazi kuupa nafasi ubabe wa kisiasa utawale. Huku waziri akiongeza
kusema:”Leo haki na kanuni zimeshinda mambo mengine yote”.”Leo, ukweli
na kanuni zimeshinda mambo mengine yote.
Dr.Riyad
Al-Maliki kwa niaba ya taifa la Palestina,amezishukuru nchi wanachama
zilizoiunga mkono Palestina katika jitihada zake,huku akitilia mkazo
kuendelea kwa nchi yake katika jitihada za kujiongezea hadhi na nafasi
mbalimbali kimataifa,ikiwa ni pamoja na kutetea haki za
Wapalestina,uhuru na amani yao kwa njia ya kidiplomasia na kisheria,
ikiwa ni pamoja na kujiunga na taasisi husika za kimataifa.
Kwa
mnasaba huu pia, Waziri Al-Maliki amesisitiza ahadi ya nchi yake ya
Palestina katika kutimiza majukumu yake ya kuchangia kupambana na
uhalifu na kuimarisha utawala wa sheria katika ngazi ya kimataifa. Huku
ikishirikiana na nchi wanachama wa Interpol katika kukuza hadhi na
nafasi ya taasisi hiyo, ushiriki wa kidhati kabisa wa kimataifa dhidi ya
uhalifu unaohatarisha maisha wananchi na mustakabali wao duniani.
Aidha
ameongeza kusema: “Nchi ya Palestina inauchukulia uanachama huu na
majukumu yake kama ni sehemu ya wajibu wake kwa Wapalestina,pia ni
wajibu wa kimaadili kwa walimwengu wote. Palestina ipo tayari na inaweza
kubeba majukumu na wajibu huu kama mshirika wa dhati katika jamii ya
kimataifa,itachangia hasa kuendeleza maadili yetu ya msingi ya pamoja
kama mataifa. ”
0 comments:
Post a Comment