Kiongozi wa upinzani, Kizza Besigye akisindikizwa na maofisa wa gereza la Luzira alikokuwa akishikiliwa
Kiongozi
wa upinzani nchini Uganda Daktari Kizza Besigye amekamatwa na polisi
jumamosi alipokuwa akitoka nyumbani kwake kasangati wilayani Wakiso.
Muda
mfupi kabla ya kukamatwa kwake Dr Besigye,kama kawaida alirushiana
maneno na mkuu wa polisi wa kituo cha Kasangati Bwana Robert Kachumu.
Daktari kizza Besigye alikamatwa baada ya kutomjibu afisa huyo wa polisi ambaye alitaka kujua Kizza Besigye anaenda wapi.
Kwa mujibu wa Daily Monitor la nchini Uganda Kizza Besigye alijitetea kuwa ana haki ya kutembea kama raia wengine.
Besigye analaani kuzuiwa nyumbani na uwepo wa askari wengi kuzunguka makazi yake.
Besigye
ambaye alikuwa mgombea uraisi kwa tiketi ya chama cha FDC alikamatwa
masaa kadhaa baada ya kundi la wanachama wa upinzani kuwaambia waandishi
wa habari kuwa wana mpango wa kuligawa bunge kufuatia kuzuiwa nyumbani
kwa kiongozi huyo.
Inaelezwa kuwa Daktari Kizza Besigye anashikiliwa katika kituo cha polisi Nagalama wilayani Mukono.RFI
0 comments:
Post a Comment