Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr.
Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino
Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano
hilo lililofanyika jana nchini Uganda.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi
wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo
na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa
gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ambae alishinda tuzo ya umahiri wa
habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi
wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.
Keki ikikatwa katika hafla hiyo
Na Mwandishi Wetu
Mwandishi
wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ameshinda tuzo ya umahiri wa
habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi
wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.
Kitabu
alikuwa anachuana na waandishi kutoka nchi za Nigeria, Burkina Faso,
Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Shindano hilo lilifanyika
jana katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyoko nje kidogo ya jiji
la Kampala.
Kwa
ushindi huo, Kitabu ambaye ni mshindi wa jumla wa shindano la Tanzania,
alijinyakulia kitita cha dola za marekani 1,500 pamoja na simu aina ya
iPhone 7+ yenye thamani za dola za Marekani 1,200.
Mwandishi
mwingine wa Tanzania aliyepata tuzo ni Koleta Makulwa kutoka Radio Free
Afrika ambaye aliwashinda waandishi wengine ambao walikuwa wanashindana
katika eneo la Radio. ambapo Tanzania ilizidi kung’ara baada ya
Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili katika waandishi
wa televisheni.
Koleta
aliondoka na kitita cha dola za Marekani 1,500, simu aina ya iPhone 7+
ya thamani ya dola za marekani 1,200 wakati Dino Mgunda alipata
zawadi ya dola za marekani 1,000 na simu ya iPhone7+ ya thamani ya
dola za marekani 1,000.
Katika
shindano hilo jumla ya waandishi 20 waliwakilisha nchi hizo. waandishi
hao ni wale ambao walikuwa washindi katika shindano la nchi mahalia,
shindano ambalo lilifanyika mwanzoni mwa wiki hii katika nchi hizo
ikiwemo tanzania.
Shindano
hilo liliandaliwa na Jukwaa la wazi la Bioteknolojia za Kilimo (OFAB)
ambalo linahamasisha matumizi ya bioteknolojia katika kilimo ili
kuwezesha nchi za Afrika ziweze kujitosheleza kwa chakula.
Mshindi
wa jumla katika shindano hilo la jana ni mtangazaji wa kituo cha TVC,
Omolara Afolayan kutoka Nigeria. Washindi waliteuliwa na jopo la majai
watano.
No comments:
Post a Comment