Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu (Kushoto) akimfatilia kwa makini Naibu waziri wa maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Wilaya ya Ikungi, Mwingine ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ikungi Ndg Elieza
Na Mathias Canal, Singida
Pamoja na
Changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi katika Jimbo la Singida
Mashariki Wilayani Ikungi Mkoani Singida lakini uhaba wa upatikanaji wa huduma
ya maji ni kikwaz kikubwa kwa wananchi kwani wanatumia umbali na muda mrefu
kutafuta maji.
Mbunge wa Jimbo la
Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu ametoa ombi hilo mbele ya Naibu waziri wa
maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya
ya Ikungi kwenye kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Mhe Miraji Jumanne Mtaturu.
Mhe Kingu alisema
kuwa Jimbo lake lina changamoto ya maji ambayo kwa kiasi kikubwa serikali
inaendeleza juhudi za kuzitatua, huku akisema kuwa katika Jimbo jirani la
Singida Mashariki linaloongozwa na Mhe Tundu Lissu hali ni mbaya zaidi katika
upatikanaji wa miundombinu ya maji kwa wananchi wake.
Alisema kuwa hivi
karibuni alipita katika jimbo hilo na kujionea adha inayowakumba wananchi jambo
amablo lilimfanya kujipanga kuwaombea maji wananchi hao katika kipindi cha
Bunge lijalo.
Alisema kuwa
wananchi hao wamebaki wakiwa utadhani hawana muwakilishi wa Jimbo kwa kipindi
cha miaka 10 jambo ambalo linafanya kuteseka na huduma za utafutaji maji kwa kutumia
muda mwingi na umbali mrefu.
Aidha, Mhe kingu
alisema kuwa pamoja na changamoto ya upatikanaji wa maji Katika Jimbo la
Singida Mashariki lakini pia jimbo hilo linakumbwa na changamoto mbalimbali
zinazoikabili sekta ya elimu ambayo ni
pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa, Nyumba za walimu, Maabara, Matundu ya
vyoo na mabweni.
Hata hivyo
alimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kwa kuanzisha
mkakati wa pamoja wa kuanzisha Mfuko wa Elimu Ikungi utakaowashirikisha
wananchi pamoja na wadau wa elimu kuchukua hatua madhubuti ili kuboresha
mazingira ya kujifunzia kwa watoto na hatimaye kuwafanya wanafunzi waweze
kuongeza ufaulu.
Naibu waziri wa
maji na Umwagiliaji Mhe Isack A. Kamwelwe ameanza ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani
Singida ambapo atatembelea na kukagua Miradi ya Maji na vyanzo vya uboreshaji
upatikanaji wa maji.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment