Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza
katika uzinduzi wa mpango mkakati wa Tanzania Evaluation Association
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizindua
mpango mkakati wa Tanzania Evaluation Association
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizindua mpango
mkakati wa Tanzania Evaluation Association
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tamisemi Mhe. Selemani Jafo
amepongeza wadau mbalimbali nchini kwa kuendelea kushirikiana na serikali
katika kuleta maendeleo ya Taifa.
Jafo aliyasema hayo alipokuwa akizindua Mpango mkakati asasi ya
watathimini nchini uitwao Tanzania Evaluation Association (TanEA) uliofanyika
Julius Nyerere Conference Centre jiji Dar es salaam.
Taasisi hiyo imefanikiwa kuzindua mpango mkakati huo wa miaka mitano
kuanzia 2017 - 2021 ambao unalenga kufanya tathmini ya mipango mbalimbali ya
maendeleo nchini ili kuweza kutoa mwanga kwa maeneo yaliyo fanyika vizuri na
maeneo ambayo hayakupata mafanikio yaliyo kusudiwa ili kuiwezesha Tanzania
kutimiza dhamira ya kufikia nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kupitia
uchumi wa viwanda.
Akizungumza katika uzinduzi huo Jafo amezitaka taasisi
mbalimbali hapa chini pamoja na taasisi za kimataifa kuendelea kushirikiana na
serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment