Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kulia, akiwahutubia wahitimu na
jumuiya ya Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)
(Hawako Pichani), wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika
katika Kituo cha Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, kulia kwake
ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA, Bw. Pius Maneno na Mwenyekiti wa Kamati
ya Elimu na Mafunzo wa Bodi hiyo, Bi. Anne Mbughuni.
Baadhi ya
wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA), wakiwa tayari kutunukiwa
shahada zao na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, katika
Mahafali ya 38 yaliyofanyika Katika kituo cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu
na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) kilichopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar
es Salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akimkabidhi cheti cha kufanya
vizuri katika masomo ya taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T), Bi. Happiness
Ngowi, wakati wa mahafali ya 38 ya Bodi hiyo yaliyofanyika Katika kituo
cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), kilichopo
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akitangaza kuwatunuku vyeti
wahitimu wa taaluma ya juu ya uhasibu (CPA-T) waliofanya vizuri katika
masomo yao, wakati wa mahafali ya 38 ya NBAA, yaliyofanyika Katika kituo
cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu, kilichopo Bunju,
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Wahitimu
waliofanya vizuri katika masomo ya NBAA, baada ya kupokea vyeti vya
kutambua umahili wao katika masomo pamoja na kupewa zawadi za fedha
taslimu zilizotolewa na wadhamini mbalimbali wa Bodi hiyo, wakati wa
Mahafali ya 38 yaliyofanyika katika Kituo cha NBAA, kilichoko Bunju, nje
kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya
wahitimu wa shahada ya Juu ya Taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa Hesabu
CPA-T, inayotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu
Tanzania (NBAA), wakila kiapo cha utii na uadilifu wakati wa mahafali ya
38 ya Bodi hiyo, yaliyofanyika katika kituo kilichoko Bunju, Nje kidogo
ya Jiji la Dar es salaam
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, (aliyeketi nafasi ya saba kutoka
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bodi pamoja na
wadhamini wa tuzo mbalimbali zilizotolewa kwa wahitimu waliofanya vizuri
katika masomo yao, tukio lililofanyika katika kituo cha NBAA, kilichoko
Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya
NBAA Prof. Isaya Jairo (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Pius
Maneno, wakiondoka kwenye viwanja vya mahafali baada ya kumaliza
kuwatunuku vyeti na shahada mbalimbali wahitimu wa kozi mbalimbali za
NBAA, katika eneo la Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (kushoto), akisalimiana na Msajili
wa Hazina Bw. Laurance Mafuru, baada ya kumalizika kwa mahafali ya 38 ya
Bodi ya taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu(NBAA), yaliyofanyika
katika kituo cha Bodi hiyo, Nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam.
Picha zote na Wizara ya Fedha
0 comments:
Post a Comment