METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, September 21, 2017

WAKULIMA: HATUKUJUA KAMA KULIMA MAHARAGWE KUNAHITAJIKA MBOLEA

Wakulima wa Kata ya Mwangoi, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakielezea namna walivyonufaika na Kilimo cha maharagwe kupitia mradi wa N2AFRICA unaojihusisha na usambazaji wa teknolojia ya mazao jamii ya mikunde hususani

Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha kitropiki wakizungumza na wakulima walionufaika na mradi wa N2AFRICA kutoka katika vijiji mbalimbali vya Kata ya Mwangoi, Wilayani Lushoto katika ukumbi wa mikutano wa kata hiyo.
Afisa Ugani wa Kata ya Mwangoi Ndg Julius Mshano akielezea namna wakulima walivyonufaika na kilimo cha maharagwe tangu Mradi wa N2AFRICA ulipoanza kazi katika kata hiyo.

Bi Nusura Omary Mkazi wa eneo na Kata ya Mwangoi Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga akionyesha miongoni mwa mafanikio aliyopo yapata kutokana na mauzo ya maharagwe kutokana na Mradi wa N2AFRICA kwa kununua pikipiki mbili zinazofanya kazi ya kubeba abiria.

Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha kitropiki wakizungumza na wakulima walionufaika na mradi wa N2AFRICA kutoka katika vijiji mbalimbali vya Kata ya Mwangoi, Wilayani Lushoto katika ukumbi wa mikutano wa kata hiyo.

Afisa Ugani wa Kata ya Mwangoi Ndg Julius Mshano akielezea namna wakulima walivyonufaika na kilimo cha maharagwe tangu Mradi wa N2AFRICA ulipoanza kazi katika kata hiyo.

Wakulima wa Kata ya Mwangoi, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakielezea namna walivyonufaika na Kilimo cha maharagwe kupitia mradi wa N2AFRICA unaojihusisha na usambazaji wa teknolojia ya mazao jamii ya mikunde hususani

Bi Nusura Omary Mkazi wa eneo na Kata ya Mwangoi Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga akionyesha miongoni mwa mafanikio aliyopo yapata kutokana na mauzo ya maharagwe kutokana na Mradi wa N2AFRICA kwa kuanza ujenzi wa nyumba ambayo imefikia katika hatua za mwisho.

Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya kilimo cha Kitropiki (IITA) Bi MaryJane na Bakari Abdallah wakizungumza na Kaimu Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Ndg Ayubu H. Omary

Picha ya pamoja kati ya Wakulima wa Kata ya Mwangoi, Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wakiwa na watafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya kilimo cha Kitropiki (IITA) mara baada ya kumalizika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kata hiyo.

Na Mathias Canal, Tanga

Wakulima wa mbogamboga na matunda Katika vijiji mbalimbali Kata ya Mwangoi Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga wamesema kuwa hawakufahamu kama kuna uwezekano mkubwa wa kulima maharagwe kwa kutumia mbolea na kupata mavuno mengi yenye tija.

Wakizungumza na wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Kitropiki (IITA) mara baada ya kuwatembelea kijijini kwao ili kufahamu namna walivyonufaika na mradi wa N2AFRICA unaojihusisha na usambazaji wa teknolojia ya mazao jamii ya mikunde, walisema kuwa mafunzo hayo na matumizi ya mbolea yameongeza ufanisi katika uzalishaji wa mazao mengi.

Wakulima hao walisema kuwa hawakuamini kama kuna uwezekano wa kutumia mbolea jambo ambalo lilipelekea kuwa na mavuno kidogo mpaka pale walipopatiwa mafunzo kupitia mradi wa N2AFRICA kuhusu matumizi ya mbolea katika zao la maharagwe.

Katika mafunzo hayo wakulima hao walinufaika pia na elimu kuhusu kulima kilimo cha kisasa ikiwemo kuacha nafasi katika mazao hayo ya maharagwe sambamba na kuondoa magugu pindi yanapoanza kuota na hatua zote za ukuaji mpaka uvunaji.

Wakulima hao wanasema kuwa mbegu bora zikiwemo Lyamungo 90, Jesca na Uyole Njano ni miongoni mwa mahitaji muhimu waliyonufaika nayo kupitia Mradi wa N2AFRICA kwani zimesaidia wakulima kupata mavuno mengi mara baada ya kulima.

Bi Nusura Omary Mkazi wa eneo na Kata ya Mwangoi Wilayani Lushoto Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mradi wa N2AFRICA akiwa mefanikiwa kununua bodaboda mbili na kukamilisha ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu.

Kwa upande wake Afisa Ugani wa Kata ya Mwangoi Ndg Julius Mshano aliomba mradi wa N2AFRICA kuongeza mbegu za mazao mengine ili wananchi waendelee kunufaika na mradi huo katika mazao mengine yenye uwezo wa kustawi katika maeneo yenye rutuba.

Mshano alisema shirika la IITA pia linaweza kuona namna ya kuwasaidia wakulima kuongeza masoko ili waweze kuuza kiwango cha soko la Kitaifa na hata kimataifa jambo ambalo litaibua chachu ya wananchi wengi kujiunga na kilimo cha maharagwe na kulifanya kuwa zao kubwa la biashara nchini.

Naye Kaimu Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga Ndg Ayubu H. Omary alisema kuwa serikali inatambua mchango wa shirika hilo kwa wakulima wa Wilaya ya Lushoto na Tanzania kwa ujumla huku akiomba juhudi ziongezwe ili kuwafikia wananchi katika maeneo yote ya Wilaya hiyo.

Omary alisema kuwa wakulima wanapaswa kuendelea kupewa mafunzo muhimu ya kuzalisha mbegu za kuazimia ili kuachana na imani za kutumia mazao ya chakula kama mbegu ilihali kuna uwezekano wa kuhifadhi mbegu.

Alisema mbolea na mbegu zinapaswa kuendelea kutolewa kwa wakati kipindi cha mwezi Octoba wakati wakulima wanaandaa mashamba kwani zikicheleweshwa inapalekea wakulima kuchelewa kupata katika kipindi husika hivyo kupunguza ufanisi katika mavuno.

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com