Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akifungua kongamano la fursa na Uwekezaji Kisarawe.
Wadau mbalimbali walioshiriki kongamano la fursa za uwekezaji
wilayani Kisarawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akiwa
kwenye picha na baadhi ya viongozi wa serikali.
WADAU mbalimbali wamejitokeza kuchangamkia fursa za uwekezaji
wilayani Kisarawe wakati wa uzinduzi wa kongamano la fursa za uwekezaji wilayani
humo.
Katika kongamano hilo limehudhuriwa na Wafanya biashara na
taasisi mbalimbali ambao wameweza kufahamu fursa nyingi ambapo hapo awali
walikuwa hawajui mazuri hayo.
Akizungumza katika ufunguzi wa kongamano hilo, Naibu waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo ameeleza kwa undani mpango wa
serikali wa viwanda sambamba na kueleza kwa kina fursa zipi zilizopo Kisarawe.
Jafo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa maelekezo yake kwa DAWASA aliyo yatoa
miezi michache iliyopita ya kupeleka maji Kisarawe na eneo la uwekezaji wa
viwanda ambapo mpango huo utachochea viwanda katika eneo la Visegese
lililotengwa kwaajili ya viwanda.
Katika eneo hilo kwasasa kuna zaidi ya ekari 1000 zilizopimwa na
kuchongwa barabara na viwanja 291 vya uwekezaji wa viwanda vikubwa na viwanda
cha kati vimeshapimwa na kutengwa tayari kwa uwekezaji.
Aidha Mpaka sasa tayari viwanda vinane vimeshajengwa ikiwa
pamoja na bandari kavu iliyopo itakayosaidia uwekezaji wa kisasa kutokana na
kupitiwa kwa reli mbili za TAZARA na Reli ya kati.
0 comments:
Post a Comment