
Wawakilishi wa Kampuni ya Jamka
Enterprise Company wakipokea hundi ya shilingi milioni Tano ambazo
wamekopeshwa na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) mara baada
ya kikao cha Wadau wa Maji na Mazingira kufunguliwa jijini Dar es
Salaam leo kwaajili ya kuzungumza masuala ya maji na mazingira.
WADAU wa maji na Mazingira washauriwa
kushirikiana ili kukidhi mahitaji ya maji kwa wakazi wa Dar es Salaam
pia washauriwa kutoa namba maalumu ya simu kwaajili ya wananchi waonapo
tatizo la maji au maji kutiririka katika maeneo mbalimbali ili kuondoa
upotevu wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam.
Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Sophia Mjema wakati akizungumza na wadau wa maji pamoja na wadau wa
Mazingira jijini Dar es Salaam leo. Amesema kuwa Wadau wamaji wanatakiwa
kushirikiana na ili kupunguza upotevu wa maji kutokana na ubovu wa
miundo mbinu ya maji.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, usambazaji
wa maji Haruni Josef Kwa upande wake DAWASCO wamewaomba wadau wa maji
ili kuendeleza na kukuza maendeleo ya kwaajili ya kujenga mtandao wa
maji kwaajili ya kuyasafirisha ili yamfikie kila mwananchi wa jiji la
Dar es Salaam.
Wadau waliokutana leo ni Mfuko wa
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wizara ya Afya, DAWASCO,DAWASA,
WATERAID na wadau wa mazingira kwa pamoja wakiwa na kauli mbiu ya maji
ni uhai na usafi ni utu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresia Mmbando akizungumza na wadau maji na usafi wa Mazingira wa
Mkoa wa Dar es Salaam, wakizungumzia masuala hasa ya maji safi na maji
taka pamoja na kutatua changamoto za maji katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
akizungumza na wadau wa maji safi pamoja na wadau wa maji taka ili
kutatua changamoto za maji katika jiji la Dar es Salaam.Pia ameshuhudia
kusaini makubaliano kati Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na
Taasisi ya Borda ya hapa nchini.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema
akishuhudia taasisi ya Borda na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
mara baada ya wadau ya maji wa maji safi na wazingira walipokutana leo
leo kufanya mazungumzo ya wadau wa maji pamoja na wadau wa mazingira.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Theresia Mmbando akibadilishana mkataba wa makubaliano kati ya ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Tasisi ya Borda kwaajili
kuendeleza na kukabiliana changamoto mbalimbali za maji na Mazingira.

Wawakilishi wa Kimchi Enterprise
Company wakipokea hundi ya shilingi milioni kumi ikiwa wamekopeshwa
na Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) jijini Dar es Salaam leo
mara baada ya kikao cha Wadau wa Mazingira kukaa kuangalia changamoto
mbalimbali zanazo kabili sekta ya maji katika mkoa wa Dar es Salaam.

Wawakilishi wa Enviromenta Management
community envelopment wakipokea hundi ya shilingi milioni kumi kwaajili
ya kuendeleza sekta ya maji pamoja na maji ambazo wamekopeshwa na Mfuko
wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) jijini Dar es Salaam leo.
kwaajili ya kuendeleza maji na mazingira katika mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya ya wadau wakiwa katika mkutano wa wadau wa maji na mazingira jijini Dar es Salaam leo.
0 comments:
Post a Comment