
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janab ameieleza Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30, 2017 kuwa moyo wa Mfanyiabiashara
Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua.

Prof. Janab ambaye ni Daktari wa moyo na
Shahidi wa kwanza upande wa uetetezi ameyasema hayo mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa
za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi,
Hajra Mungula, alisema yeye ni Daktari wa moyo wa Taasisi ya JKIC.
Amesema anamfahamu Manji baada ya
kufikishwa katika Taasisi hiyo February 2017 akiwa mwenye matatizo ya
moyo na kuongeza kuwa alipofikishwa hapo alifanyiwa vipimo na jopo la
madaktari lililobaini Moyo wake umewekewa vyuma ambapo akaingizwa mipira
maalum na kubaini kwamba upo katika hali nzuri.
”July 2017 alirudishwa tena katika
Taasisi yetu akiwa na tatizo hilo la moyo pamoja na maumivu ya mgongo na
kutokuwa na usingizi.”
Prof. Janab amesema alivyorudi hapo
walimpokea kama mgonjwa aliyetibiwa nje ya nchi na ripoti ilionyesha
ametibiwa Florida, Marekani.
Alipoulizwa na Wakili Mungula kama
mgonjwa aliyewekewa vyuma katika moyo anaweza kutumia dawa za kulevya,
Prof. Janab alijibu kwamba huwa haruhusiwi kufanya baadhi ya mambo
ikiwemo kuvuta sigara, kutumia Heroin.>>>”Hivyo kama akitumia
athari zake ni kwamba mirija ya moyo itaziba, kisha atatakiwa afanyiwe
upasuaji mkubwa zaidi.”
Prof. Janab ameongeza kuwa katika awamu
ya pili ya Manji kurudi hospitalini hapo walimsaidia kumtibia maumivu
aliyokuwa nayo kwa kumpa Drip ya Paracetamol’s na Sindano ya Tram a do.
Akijibu hoja ya Wakili wa Serikali,
Timony Vitalis kwamba matumizi ya dawa za kulevya yanaweza kusababisha
ugonjwa wa moyo, Prof. Janab alijibu ndio.
Kesi imeahirishwa hadi August 31, 2017 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
0 comments:
Post a Comment