Mkulima wa zao la maharagwe Kitongoji cha Dukani, Kijiji na Kata ya Baga, Wilaya ya Bumbuli Ndg Ismail Abasi akionyesha mbuzi wa maziwa aliowanunua kutokana na mafanikio mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.
Mkulima wa zao la maharagwe Kitongoji cha Dukani, Kijiji na Kata ya Baga, Wilaya ya Bumbuli Ndg Ismail Abasi akionyesha Ng'ombe wa maziwa aliowanunua kutokana na mafanikio mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.
Mwandishi wa habari Mwandamizi na Mhariri wa Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Ndg Mathias Canal (Kulia) alipomtembelea Mkulima wa zao la maharagwe Kitongoji cha Dukani, Kijiji na Kata ya Baga, Wilaya ya Bumbuli Ndg Ismail Abasi (Wa Pili Kulia) kujionea Ng'ombe wa maziwa aliowanunua kutokana na mafanikio ya mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.Wengine ni Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Kitropiki (IITA) Ndg Bakari Abdallah na Bi MaryJane Clemence
Mkulima wa zao la maharagwe Kitongoji cha Dukani, Kijiji na Kata ya Baga, Wilaya ya Bumbuli Ndg
Ismail Abasi (Wa Pili Kulia) akielezea jinsi alivyonufaika na mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.
Afisa Kilimo
wa Kata ya Baga Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Ndg Elisafi Mashauri Mbaga akielezea jinsi wakulima wa maharagwe walivyonufaika na mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.
Afisa Kilimo
wa Kata ya Baga Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Ndg Elisafi Mashauri Mbaga (Kulia) akielezea jinsi wakulima wa maharagwe walivyonufaika na mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe.Wengine ni Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Kitropiki (IITA) Ndg Bakari Abdallah na Bi MaryJane Clemence
Wataalamu wa utafiti kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa kilimo cha Kitropiki (IITA) wakiwa kazini Wilaya ya Bumbuli kuwatembelea wananchi kuona namna walivyonufaika na Mradi wa N2AFRICA
Athumani Ismail mtoto wa Mkulima wa zao la maharagwe Kitongoji cha Dukani, Kijiji na Kata ya Baga, Wilaya ya Bumbuli Ndg
Ismail Abasi akielezea jinsi alivyonufaika na mradi wa N2AFRICA katika kilimo cha maharagwe kwa kulipiwa ada na hatimaye sasa kuelekea kujiunga na chuo kikuu.
Mkulima
Ismail Abasi akionyesha jinsi alivyoboresha nyumba yake kutokana na mradi wa N2AFRICA katika
kilimo cha maharagwe.
Na Mathias Canal, Tanga
Wakulima wadogo
wameuomba mradi wa N2AFRICA unaojihusisha na usambazaji wa teknolojia ya mazao
jamii ya mikunde hususani maharagwe kuwasaidia mbegu zingine ili kuongeza
uzalishaji wa mazao mengi kwa manufaa kama ilivyo katika zao la awalila
maharagwe walilopatiwa mbegu na elimu bora ya kilimo.
Mradi huo ambao upo
chini ya Taasisi ya Kimataifa ya utafiti wa Kitropiki (IITA) umesaidia wakulima
Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga kupata elimu ya kilimo bora kupanda kwa kuacha
nafasi, Kutumia mbegu bora na kulima maharagwe kwa kutumia mbolea tofauti na
walivyokuwa wakilima kabla ya mradi huo.
Akizungumza kwa niaba
ya wakulima wengine wanufaika wa mradi huo Ndg Ismail Abasi aliomba kuongezwa
mbegu nyingi za kilimo jamii ya mikunde ambazo ni pamoja na maharagwe yenyewe, kunde,
mbaazi, karanga, soya, na choroko kwani ni mazao ambayo yanastawi kwa wingi
katika maeneo hayo ya baridi.
Alisema katika
nchi mbalimbali Barani Afrika ikiwemo Tanzania, upotevu wa mazao mashambani ni
karibu asilimia 25 Kati ya mavuno yaliyotarajiwa kuvunwa hupotea huku robo tatu
ya mavuno yote ambayo hupatikana salama.
Alisema hiyo robo
tatu ya mavuno, nayo hubaki ikiwa shakani kutokana na wadudu waharibifu
na kuhifadhiwa katika maghala ambayo yapo chini ya kiwango.
Alisema japo mradi
huo wa N2AFRICA umewasaidia wakulima kulima kitaalamu lakini wanapaswa kuongeza
ufanisi kwa kutoa viuatilifu kwa ajili ya kuuwa wadudu shambani kwani vilivyopo
vinauzwa gharama kubwa ambazo sio rahisi wakulima wote kuzimudu.
Aliongeza kuwa Baadhi
ya mazao, kama vile matunda, mboga za majani na mazao ya mizizi yanapotea
mashambani kwa asilimia 50, ikiwa ni mavuno yote ambayo
yalitarajiwa kuvunwa hivyo ni hatari kwa mkulima kutokana na nguvu nyingi
anazowekeza shambani lakini mavuno yanakuwa kidogo.
Akizungumzia jinsi
wakulima walivyonufaika na mradi huo tangu ulipoingia Wilayani Bumbuli Afisa Kilimo
wa Kata ya Baga Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Ndg Elisafi Mashauri Mbaga alisema
tangu wakulima walipopatia mafunzo ya namna ya kuboresha kilimo chao ikiwemo
kutumia mbegu na mbolea bora wamebadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa wapo
waliofanikiwa kwa kuwalipia ada watoto wao, kufanya marekebisho ya nyumba zao,
kununua bodaboda, kuboresha mazingira ya ndani ya nyumba na kuwa na kipato cha
kukidhi mahitaji muhimu ya binadamu.
Alisema pamoja na mambo mengine yupo
adui mkubwa kwenye zao la maharagwe kwa wananchi katika vijiji mbalimbali Katika
Kata hiyo ikiwa ni pamoja na madoa pembe, na kutu.
Hata hivyo alisema kuwa magonjwa
yanayo sababishwa na bakteria na virusi punguza magonjwa hayo ni kupanda mbegu
safi, aina zinazo vumilia na kutunza shamba na unaweza kutumia madawa kama kocide,
fugulani, Bayleton kwa kuzuia magonjwa yanayosababishwa na ukungu na
bakteria.
Mradi wa N2AFRICA unaendeshwa na na Taasisi ya Kimataifa ya kilimo cha Kitropiki katika ukanda wa joto makao makuu yake ni nchini Nigeria chini ya ufadhili wa Bill na Melinda Gates na kuongozwa na Chuo Kikuu cha Wagenigen cha Uholanzi.
Mradi wa N2AFRICA unaendeshwa na na Taasisi ya Kimataifa ya kilimo cha Kitropiki katika ukanda wa joto makao makuu yake ni nchini Nigeria chini ya ufadhili wa Bill na Melinda Gates na kuongozwa na Chuo Kikuu cha Wagenigen cha Uholanzi.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment