METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, August 25, 2020

NEC YATANGAZA WATANO KUWANIA UBUNGE ILEMELA

 Tume ya uchaguzi (NEC) Jimbo la Ilemela imetangaza wagombea wa vyama vitano waliokidhi vigezo kuwania nafasi ya ubunge wa jimbo hilo baada ya vyama 14 kujitokeza, 3 vikishindwa kurejesha fomu ya uteuzi.

Akizungumza mara baada ya mchakato wa kupitia fomu za wagombea, Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Ilemela Ndugu John Wanga amesema kuwa katika Jimbo la Ilemela jumla ya vyama kumi na nne vilijitokeza kuchukua fomu ya kuwania uteuzi wa nafasi hiyo, Na vyama vitatu havikurejesha fomu ya uteuzi huku vyama 11 vikirejesha fomu ya uteuzi na mara baada ya kuzipitia fomu hizo vyama  vitano pekee na wagombea wake walikizi vigezo na kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kikiwemo Chama Cha Mapinduzi mgombea wake akiwa Ndugu Dkt Angeline Mabula, Chama Cha ADC mgombea wake akiwa Ndugu Shabani Haji Tutu, Chama Cha ACT Wazalendo mgombea wake akiwa Ndugu Mkiwa Adam Kimwanga, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo mgombea wake akiwa Ndugu Greyson Wanzagi na Chama Cha Demokrasia Makini mgombea wake akiwa Ndugu Ahmed Juma Kusanya wakati Chama cha DP, CUF, CCK, NRA, SAU na NCCR Mageuzi wagombea wao wakienguliwa kwa kutokidhi vigezo na masharti ikiwemo kukosa wadhamini na kutolipa dhamana ya uteuzi

‘... Kazi tunayoifanya ni kwa mujibu wa sheria na leo tunatangaza wagombea waliokidhi vigezo vya uteuzi kwa nafasi ya ubunge, Kwa jimbo la Ilemela waliochukua fomu ya kuomba uteuzi walikuwa wananchi 14  ...’ Alisema

Aidha Ndugu Wanga akaongeza kuwa wagombea walioteuliwa wanaweza kuwekewa pingamizi kwa msimamizi wa uchaguzi ndani ya masaa 24 mara baada ya kutangazwa kwa wagombea hao huku akisisitiza kuwa zoezi la kuteua wagombea wa vyama vya siasa kwa nafasi hiyo lilikuwa la uwazi, huru na haki kwa misingi ya sheria na katiba bila kumuonea mtu yeyote.

Kwa upande wake moja ya wagombea walioteuliwa kutoka Chama Cha Mapinduzi Ndugu Dkt Angeline Mabula ambae pia alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa awamu iliyokwisha mbali na kushukuru kwa kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) akawataka wanachama wa chama chake waliojitokeza kumsindikiza  kumuamini na kumuunga mkono mgombea wa nafasi ya Urais wa chama hicho Ndugu Dkt John Magufuli huku akiwaahidi kuendelea kuwatumikia kwa kuhakikisha wanapata maendeleo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com