Katibu mkuu wizara ya Maliasili na Utalii Dr Aloyce Nziku akikagua Gwaride liloandaliwa na jeshi USU kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA Mara baada ya kutembelea Makao makuu yake yaliyopo Kingolwira Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akisalimiana na maafisa wa TAWA Mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce K.Nzuki akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika ofisi za TAWA Mkoani Morogoro.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Aloyce K.Nzuki ametembelea Ofisi za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) zilizopo eneo la Kingolwira, mjini Morogoro.
Aidha Amefanya kikao na Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Afande Mabula N. Misungwi katika ofisi yake kujadili namna bora ya utekelezaji wa shughuli za Mamlaka hiyo.
sambamba na hilo viongozi hao kwa pamoja wamejadili namna bora ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo (TAWA) iliyo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Awali akiingia katika ofisi hizo za TAWA alipokelewa na gwaride la askari wa Jeshi usu kutoka TAWA na alikagua gwaride hilo ambalo lilikuwa limeandaliwa rasmi kwa ajili yake.
Pamoja na ukaguzi huo vile vile alisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Menejimenti waliopo Makao Makuu.
0 comments:
Post a Comment