Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja
na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi
wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi
mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka
jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia
jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi
Kigoma na Mwanza.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama
Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja
Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard
Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye
kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth
Magufuli pamoja na Hawa Ghasia (Mb). Picha zote na IkuluRais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati
akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli anastahili pongezi na heshima kubwa sio dhihaka, Ghubu na ghila za baadhi ya watanzania kutokana na kazi kubwa anazozifanya kwa manufaa ya kizazi cha sasa nchini Tanzania na kizazi kijacho.
Rc Makonda ameyasema hayo mbele ya Rais na watazania alipokuwa akitotoa salamu za Mkoa wa Dar es salaam wakati wa dhifa ya kuweka jiwe la msingi uzindua wa ujenzi wa Reli ya kati mpya na ya kisasa ya umeme (Standard Gauge) sehemu ya Dar es salaam hadi Morogoro.
Tukio la uzinduzi limefanyika katika Stesheni ya Pugu Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam na ujenzi utakapokamilika Treni hiyo itakuwa na uwezo wa kusafiri Kilomita 160 kwa Saa moja.
Rc Makonda alisema kuwa haijawahi kutokea katika historia ya Taifa la Tanzania kuwa na Reli na Treni yenye uwezo wa kwenda kwa spidi kubwa kama ambavyo imezinduliwa ujenzi wake na kuleta manufaa kwa Taifa la Tanzania na watanzania wote.
Makonda Alisema kuwa Rais anapaswa kupongezwa kwa dhati kabisa kwani Moja ya ahadi zakilikuwa ni kujenga barabara za juu kwenye jiji la Dar es salaam kwenye maeneo ya Ubungo na TAZARA na Siku ya Jumamosi tarehe 16 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais aliweka jiwe na msingi la ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya barabara Nyerere na Mandela (Flyover ya TAZARA).
Jumanne tarehe 19 Aprili, 2016 Mheshimiwa Rais alifungua rasmi Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680 na barabara unganishi (approach roads) upande wa Kurasini na Kigamboni zenye urefu wa kilometa 2.5. Ujenzi uliofanywa na Kampuni ya China Railway 15 Group ilishirikiana na Kampuni ya China Bridge Engineering Group.
Aidha Jumatatu ya Machi 20, 2017 Rais Dkt John Pombe Magufuli, alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu (fly-over) eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo aliweka jiwe la msingi na kuzindua ujenzi huo. Fly-over hiyo inatarajiwa kupunguza kero ya msongamano wa magari eneo la Ubungo na sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam.
Rc Makonda alisema kuwa Sambamba na ujenzi wa barabara za juu (fly-over) eneo la Ubungo na TAZARA pia Rais Magufuli atajenga daraja la Salender, ambapo Daraja hilo la Salender litakuwa na urefu wa kilometa 7 zikiwemo kilometa 1.4 zitakazopita baharini.
Katika upande mwingine RcMakonda amesema kuwa watu wote wanaolia kuhusu utendaji wa Rais Magufuli ni wale waliokuwa wapiga dili, Wala Rushwa, Mafisadi na wanaojishughulisha na dawa za kulevya hivyo kutokana na jinsi walivyobanwa na serikali ya awamu ya tano ni lazima walie na serikali haitojali kilio chao kwani serikali inapaswa kuwa na manufaa na kufurahisha wananchi wote sio wapiga dili wachache.
Mkuu huyo wa mkoa wa Dar es salaam amewataka waandishi wa habari kote nchini kwa kauli moja kufanya kazi yenye manufaa ya kujenga Taifa kwani kufanya hivyo watakuwa wametumia taaluma zao ipasavyo kulikokueneza chuki na uchonganishi.
Amesema kuwa kwa kiasi kikubwa amekuwa akishangazwa na kutokuwepo kwa habari zenye maslahi ya Taifa katika vyombo vya habari hivyo hatoshangaa kutoona habari ya uzinduzi wa ujenzi wa Reli ya kati mpya na ya kisasa ya umeme (Standard Gauge) sehemu ya Dar es salaam hadi Morogoro.
Hata hivyo RcMakonda alisema kuwa kumekuwa na hofu na watu wakihoji juu ya ufanyaji kazi wa Mkuu wa Mkoa kuhusu kupambanana Dawa za Kulevya, watu hao wanapaswa kusoma mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.
kwa mujibu wa kifungu 61 (4) na (5) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vifungu 5, 6na 7 vya sheria ya Tawala na mikoa Na 19 ya mwaka 1997, Mkuu wa Mkoa ana wajibu wa kusimamia kazi na shughuli zote za serikali ya Muungano wa Tanzania katika Mkoa aliokabidhiwa. Atatekeleza kazi na shughuli zote zilizotajwa na sheria au kwa mujibu wa sheria kama ni kazi au shughuli za Mkuu wa Mkoa na atakuwa na madaraka yote yatakayotajwa na sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment