METDO Tanzania

METDO Tanzania

Sunday, May 14, 2017

MKURUGENZI WA MANISPAA YA UBUNGO NDG JOHN LIPESI KAYOMBO ATOA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU MZEE SOZIGWA ALIYEWAHI KUWA MWANDISHI WA HAYATI MWL J.K NYERERE

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa familia ya Marehemu Mzee Sozigwa Mtaa wa Mtoni Mtongani Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa pole kwa mke wa Marehemu Mzee Sozigwa Mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Mtoni Mtongani Jijini Dar es salaam

Na Mathias Canal.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo Mei 14, 2017 amezuru kutoa pole kwa Katibu wa Afya Manispaa ya Ubungo Bi Lucy Paul Sozigwa aliyefiwa na baba yake Mzazi Marehemu Mzee Paul Andreas Ruben Sozigwa.
Marehemu Mzee Sozigwa alifariki Dunia usiku wa kuamkia Mei 12, 2017 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Moyo uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Mazishi ya Marehemu Mzee Sozigwa yatafanyika Jumanne Mei 16, 2017 katika Kijiji cha Sanze Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
Marehemu Mzee Sozigwa enzi za uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini na Kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambapo aliwahi kuwa Mwandishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Amewahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, pia amewahi kuwa Katibu Mkuu wa shirika la Reli Tanzania.
Katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) Marehemu Mzee Sozigwa amewahi kuwa Katibu wa kamati ya Nidhamu na Maadili, Pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa kampeni za uchaguzi wa CCM Wakati katika kipindi cha Awamu ya nne.
Mpaka kifo kinamkuta Marehemu Mzee Sozigwa ameacha watoto sita ambapo kati yao watoto wa kiume ni wanne na Watoto wa Kike ni wawili.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com