METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 15, 2017

MBUNGE WA ILEMELA AWAFUNDA WAHITIMU DIT

Na Ofisi ya Mbunge

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameshiriki sherehe za mahafali ya kwanza kwa wahitimu wa chuo cha DIT Kampasi ya Mwanza waliomaliza  mafunzo ya utengenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi sherehe ambazo zilihudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt Leonard Masale na Mkurugenzi wa Ilemela John Wanga

Akizungumza katika mahafali hayo  yaliyohusisha jumla ya wanafunzi Tisini kutoka mikoa yote ya Tanzania na kutanguliwa na ukaguzi wa miundombinu na shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho Dkt Mabula amewataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo waliyoyapata kama chachu ya kujikwamua kiuchumi kwa kuanzisha vikundi vinavyosaidiika na serikali kama njia ya kuyafikia malengo ya serikali ya Tanzania ya Viwanda

‘… Huwezi kuwa na Tanzania ya viwanda kama huna watumishi wakufanya kazi katika viwanda hivyo,Mnaowajibu wa kuyatumia mafunzo mliyoyapata kama njia ya kuifikia Tanzania ya Viwanda na niwaambie tu malengo ya Afrika Mashariki ni kuacha kutegemea bidhaa za viatu kutoka nje hivyo mkijiunga katika vikundi mtasaidiika kiurahisi …’ Alisema

Aidha amekemea tabia ya vijana kuchagua kazi huku  akiasa kutumika kwa kila fursa inayojitokeza

Akimkaribishwa mgeni rasmi Mkuu wa chuo hicho Dkt Albert Mmari mbali na kushukuru amesema kuwa taasisi yake itaendelea kuwa dira katika kutekeleza kwa vitendo uelekeo wa serikali juu ya kutimiza ndoto ya nchi ya viwanda huku akitaka wadau mbalimbali kujitokeza  kuunga mkono jitihada zinazofanywa

Akihitimisha  Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu Ndugu Gabriel Saelie amesema kuwa kinachofanyika ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi inayotaka kukuza ujuzi ili kukabiliana na changamoto ya ajira kunakoenda sambamba na ufunguaji wa viwanda vidogo sanjari na kuwataka watu wa kanda ya ziwa kutumia vizuri malighafi za ngozi zinazopatika kwa wingi katika kujikwamua kiuchumi

Wakati huo huo Naibu Waziri Angeline Mabula ameshiriki ufungaji wa mafunzo ya siku tatu ya Ujasiriamali yaliyofanyika katika kanisa la Baptist lililopo Kona ya Bwiru yaliyokuwa yakitolewa na taasisi ya Integrity kwa kushirikiana na Manispaa ya Ilemela ktk kuhakikisha wananchi wanakuwa na elimu ya kutosha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuacha utegemezi

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ‘

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
15.05.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com