Na Mwandishi Wetu, Mwanza
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi ameipongeza na kuisifu Manispaa ya Ilemela kwa Kasi yake ya Maendeleo sambamba na Utaratibu wake wa kutatua Migogoro ya Ardhi kwa wananchi
Hayo ameyasema wakati wa Ziara yake ya kikazi ndani ya Manispaa hiyo iliyohusisha Ukaguzi wa mifumo inayotumika kulipia kodi ya ardhi, Kikao cha ndani kilichojumuisha madiwani, viongozi wa wilaya, mkoa na wataalamu wa ngazi zote na baadae kufanya Mkutano wa hadhara kata ya Mecco unapofanyika Mradi wa Urasimishaji makazi na kuzungumza na Wananchi wa eneo hilo na maeneo jirani waliojitokeza kumsikiliza
‘… Hakuna manispaa yeyote yenye uwezo wa kuendelea kwa haraka na muda mfupi kama nyinyi, Nilikuja hapa mara ya mwisho ni tofauti na nilivyowakuta leo nilikuwa nawaza kuwanunulia mashine za RTK nchi nzima lakini nyinyi mmeweza kununua wenyewe maanake mmekuwa juu ya wazo langu na juzi marafiki zenu wa Korea nmesaini barua wanakuja na mfumo wa uboreshaji na usimamizi wa ardhi …’ Alisema
Aidha Mhe Lukuvi ameongeza kuwa ipo haja ya kufundisha manispaa nyengine utataribu unaotumika katika kutatua migogoro ya ardhi nakuahidi kuwa yupo teyari kusaidia mawasiliano na wizara nyengine unapotokea uhitaji kwa migogoro itakayohusisha taasisi zaidi ya moja huku akitaka kutafuta namna nyengine ya kuhakikisha juhudi katika ukusanyaji wa kodi za ardhi na utoaji wa hati zinaongezeka ili kuiongezea nchi pato litalosaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo
Kwa upande wake mkuu wa mkoa Mwanza Mhe John Mongela mbali na kumshukuru kwa kuutembelea mkoa wake mara kwa mara hasa Ilemela ameahidi kuiga mfano wake kwa kurudi Ilemela kutatua changamoto za ardhi zitazoshindikana kwa ngazi ya wilaya
Wakihitimisha kwa wazo la pamoja mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Dkt Leonard Masale, Meya wa manispaa hiyo Mhe Renatus Mulunga na Mkurugenzi wake Ndugu John Wanga wamemuhakikishia kuwa watatekeleza maelekezo yote
aliyoyatoa katika ziara yake haraka iwezekanavyo sambamba na kumpongeza Naibu Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dkt Angeline Mabula katika kusaidia utatuzi wa changamoto za ardhi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo
Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
29.04.2017
0 comments:
Post a Comment