METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, May 1, 2017

DC HOMERA APOKEA MIFUKO 100 YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA NAKAYAYA

Na Mwandishi Wetu, Ruvuma

Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera amepokea mifuko mia moja ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne Tshs 1,400,000/= toka kwa wadau wa maendeleo wilayani Tunduru.

Mifuko hio ya saruji imetolewa na Bw. Emmanuel Magohi na Bw. Methoy Ngonyani kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkuu wa wilaya ya Tunduru.

Akizungumza kwa niaba ya mwenzie Bw. Emmanuel Magohi alisema, wanatoa mifiko mia moja ya saruji kwa kuonesha imani yao  kwa juhudi anazofanya Mkuu wa wilaya Mhe. Juma Homera.

Dc Homera alisema, anawashukuru sana Bw. Ngonyani na mwenzake kwa kuunga mkono jitihada zake za kujenga kituo cha Afya Nakayaya, na pia alitumia fursa hio kuwaomba wadau wengine wajitokeze ili waweze kushiriki ujenzi wa kituo hicho kwa kuwa kinajengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe.

Hadi sasa kuna mifuko mia sita 600 ya saruji na shilingi milioni sita 6,000,000/= tukijumlisha pamoja na ahadi ila fedha taslim ni shilingi milioni tatu na laki mbili Tshs. 3,200,000/= michango bado inapokelewa.

Zoezi la ufyatuaji wa matofali bado linaendelea na hadi muda huu tumefikisha matofali zaidi ya elfu mbili 2000 ya nchi sita na ujenzi wa msingi wa moja ya majengo nane unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Aidha, Mhe. Homera alimkabidhi kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Jonathan Haule mifuko hio na kumsisitizia isitumike kimyume na matakwa yaliyokusudiwa  kwa kuwa atakuwa anafuatilia kwa ukaribu Matumizi ya siment.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com