Waziri wa Madini Doto Biteko katikati na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakiangalia kitu wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara, Ihumwa.
Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.
Waziri wa Madini Doto Biteko, (mwenye koti) Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) na Prof. Simon Msanjila (mwenye tisheti nyekundu) wakikagua maeneo maeneo mbalimbali ya jengo la Wizara
v Waziri Biteko asema wizara iko
tayari kuwahudumia watanzania kutokea Ihumwa
v
Mkandarasi
aahidi kukamilisha ujenzi ndani ya siku Tano
Viongozi
Waandamizi wa Wizara ya Madini, wakiongozwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko
leo Machi 23, wametembelea Jengo la Wizara ya Madini lililopo mji wa Serikali
eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Akizungumza
baada ya kukagua jengo hilo, Waziri wa Madini Doto Biteko amewahakikishia
watanzania wote pamoja na wadau wa madini kuwa, wizara iko tayari kuwahudumia
kutokea eneo hilo la Ihumwa pindi itakapohamia na kuwataka watumishi kujiandaa
kuhamia eneo hilo mara baada ya mkandarasi kukabidhi jengo kwa wizara.
Vilevile,
Waziri Biteko amezitaka taasisi nyingine zenye uhitaji wa kutumia madini ya
mawe yanayopatikana nchini ikiwa ni pamoja na mable, kuwa wizara iko tayari kuwasaidia kwa kuwaunganisha na
wajeta wake.
Pia,
amemshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa kutokana
na msukumo alioutoa kuhakikisha ujenzi wa majengo ya serikali unakamilika kwa
wakati.
Aidha,
amempongeza Mkandarasi kampuni ya Mzinga
Holding Co. Ltd kutokana na kuongeza kasi ya ujenzi ikiwemo kuzingatia ubora
nakuongeza kwamba, wizara imeridhika na ujenzi.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, ameeleza kuwa, wizara
imepanga kulifanya eneo la ofisi hiyo kuwa kijani kwa kuhakikisha inapanda miti
ya aina mbalimbali na kuhakikisha kwamba eneo hilo linawekewa mazingira mazuri
ya kuvutia.
Naye,
Katibu Mkuu wa Madini, Prof. Simon Msanjila Amesema Mkandarasi Kampuni ya
Mzinga Holding Co. Ltd imeahidi kuikabidhi Wizara jengo hilo ndani ya kipindi
cha siku Tano zijazo “awali ujenzi ulianza kwa kusuasua lakini sasa uko katika
hatua nzuri na mkandarasi amezingatia ubora,” amesema Prof. Msanjila.
Akizungumzia
mahitaji ya ofisi na idadi ya watumishi, amemsema kwa idadi ya watumishi wa
wizara Makao Makuu ofisi zilizopo katika jego hilo zinatosheleza mahitaji na
kuongeza kuwa, kwa kuanza Idara zote na Vitengo vya Wizara vinatarajia kuhamia
katika eneo hilo isipokuwa Idara ya fedha kutokana na masuala ya mfumo wa
kifedha.
Pia,
ameeleza kuwa, wizara imetumia malighafi inayopatikana nchini yakiwemo madini
ya mable ambayo yamepatikana kutoka
kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini.
Kwa
upande wake, Mkandarasi wa kampuni hiyo Hamisi Msangi ameihakikishia wizara kuwa , ndani
ya siku tano zijazo, jengo hilo litakabidhiwa rasmi kwa wizara hiyo.
0 comments:
Post a Comment