Asasi za kiraia
12 zilizo chini ya ufadhili wa ubalozi wa Ufalansa na kusimamiwa na Taasisi ya
Foundation for Civil Society zimekutana kutathmini miradi kadhaa ya maendeleo
ya jamii wanayoitekeleza katika mikoa mbalimbali.
Akiongea na
waandishi wa habari mach 21, 2019 katika Hotel ya Protea Cortyard iliyopo Oyster bay jijini Dar es salaam, Meneja Uwezeshaji wa FCS
Bi. Edna Chilimo amesema kuwa lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini na kuona
mradi huo umefanikiwa kiasi gani na umekuwa na changamoto zipi, pamoja na
kutafuta ufumbuzi ili awamu ijayo waweze kufanya vizuri zaidi.
Aliongeza kuwa mradi huo ulipewa fedha na Ubalozi wa Ufalansa hapa nchini na ulikuwa na programu mbili ambazo PISSCA na DEFI na programu hizo zote zimelenga kujenga uwezo wa mitandao ya Asasi za Kirai na kuboresha baadhi ya maeneo katika jamii.
Aidha
alisema kuwa mradi huo ulikuwa ni wa miaka miwili na huu ni mwaka wa mwisho, Lakini pia
ulihusisha asasi 12 za Tanzania bara na uliweza kuleta mafanikio makubwa kwa
jamii hasa kwa upende wa afya ya uzazi kwa watoto wa kike na wakiume ambapo
watekelezaji wakubwa katika hili walikuwa ni Msichana Initiative.
Aliongeza
kuwa kuisha kwa mradi huu siyo mwisho na kuwashauri wadau watengeneze miradi
yenye matokeo mazuri yaani inasaidia jamii hasa ile ya watu wa chini na
kuongeza ubunifu juu ya kile wanachokifanya ili kuwashawishi wafadhili kwani
wafadhili wengi wanapenda kuona fedha wanazotoa zinaleta mabadiliko chanya kwa
jamii.
Kwa upande
wake Lightness Njau kutoka Taasisi ya
Msichana Initiative alisema kuwa wao waliufanya mradi huo katika wilaya mbili
za Mji wa Dodoma ikiwemo Wilaya ya Kongwa na Chamwino, Na walilenga shule mbalimbali
za msingi na sekondari katika wilaya hizo, walichokifanya ni kufungua Clabs mashuleni na katika club hizo
10 zilikuwa za shule za msingi na 32 za shule za sekondari.
Aliongeza
kuwa mafanikio waliyoyapata kutoka katika club hizo mpaka sasa ni wasichana
katika shule hizo wameweza hata kuzidai na kuzizungumzia haki zao za msingi,
Lakini pia wasichana wengi kwenye hizo club wameweza pia kuwaelimisha wenzao
ambao hawapo katika club kuhusu madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Alisisitiza
kuwa kwa hizo wilaya zote mbili pamoja na kata sita waliweza kufungua Kamati za
Ulinzi wa wanamke na Mtoto na zimeanza kuleta matokeo mazuri kwa kuwa mpaka sasa
taarifa mbalimbali wanazipokea kutoka kwa wanajamii, Lakini pia wanapewa
usharikiano mzuri na serikali katika wilaya hizo zote.
Na kwa
upande wa shirika la TAWLA wao waliweza kutekeleza mradi huu kwa kufanya kazi
katika eneo la ukatili wa kijinsia kwa kuwajengea uwezo Polisi na Wasaidizi wa
kisheria pamoja kuwapa msaada wa kisheria kwa waathirika wa vitendo vya
ukatili.
Lakini pia
kufatia mchakato huo zaidi ya wanawake 472 wameweza kupatiwa msaada na
wasaidizi wa kisheria katika wilaya ya Bayo na Mpwapwa, Na kwa upande wa polisi
walijengewa uwezo kuzitilia uzito kesi za ukatili wa kijinsia na kuhakikisha
zinafikishwa Mahakamani pale ushahidi unapokamilika na kuacha tabia ya
kuzipuuzia.
Akionge kwa
niaba ya Taasisi hiyo Bw. Barnabas Kaniki alisema kuwa changamoto kubwa katika
mradi huo ilikuwa muda ni mdogo kwa kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia
haviwezi kumalizika kwa mwaka mmoja au miwili, Lakini pia changamoto nyingine
ni fedha zilizotengwa hazikuweza kufanikisha kufika katika kata zote za wilaya
hizo.
Na taasisi zilizokuwa zikitekeleza mradi huo ni IWAPOA, Dignity Kwanza, ATFGM, NGONEDO, NGSEN, GLT, TEG, UWZ, TAWLA, TAMWA, Msichana Initiative na CDF.
Meneja Uwezeshaji wa FCS Bi. Edna Chilimo Akiongea na waandishi wa habari juu ya dhumuni la mkutano.
Lightness Njau kutoka Taasisi ya Msichana Initiative akitoa wasilisho juu ya mradi wao uliolenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa shule mbalimbali Mkoani Dodoma
Washiriki wakiendelea na mkutano.
Muwakilishi wa Taasisi ya TAWLA Bw. Barnabas Kaniki akitoa mchanganuo juu ya mradi waliyoufanya wao ambapo waliangazia katika kuwakomboa wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mkutano.
Mkutano ukiendelea.
0 comments:
Post a Comment