Madaktari walio katika mgomo nchini
Kenya wanomba nyongeza ya mshahara ya 50% kama ilivyokubaliwa katika
mkataba uliosainiwa mwaka 2013.
Kutokana na kutopatiwa suluhu
yoyote katika mazungumzo na madaktari wa Kenya walio katika mgomo, Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta alitoa maneneo makali Jumanne wiki hii
akiwashambulia madaktari takriban 5,000 madaktari wa hospitali za umma.
Kufuatia kuzorota kwa shughuli katika
vituo vya afya vya umma, serikali imetishia kuajiri madaktari kutoka
Cuba watakaochukua nafasi za madaktari wanaoendelea na mgomo.
Madaktari walio katika mgomo nchini
Kenya wanomba nyongeza ya mshahara ya 50% kama ilivyokubaliwa katika
mkataba uliosainiwa mwaka 2013, lakini makubaliano hayo hayajatekelezwa.
Mpaka sas serikali imekua ikipendekeza nyongeza ya mshahara ya 40%.
Madaktari walio katika mgomo pia
wanalalamikia rushwa ambayo imekithiri nchini Kenya na wanaomba
marupurupu ya ziada kwa hospitali za umma.
Inaarifiwa kwamba chama cha madaktari kimesaini hati ya kumaliza mgomo na wameiomba serikali kufanya hivyo.RFI
0 comments:
Post a Comment