Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga, Naibu Mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa na Mhe Omary Mgumba, pamoja na wataalamu wa wizara ya kilimo wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Pichani ni Naibu mawaziri wa kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Kulia) na Mhe Omary Mgumba, wakifatilia kikao kazi kilichoongozwa na Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga wakizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akimsikiliza mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke akizungumza kwenye kikao kazi wakati alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma, Jana tarehe 4 Januari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. SARAH
COOKE, jana tarehe 4 Januari 2019 amemtembelea Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga na kufanya nae
mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya Tanzania
na Uingereza katika sekta ya kilimo.
Katika mazungumzo hao, Mhe Hasunga na Bi. COOKE wamekubaliana kuongeza kasi ya
Ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, makubaliano ambayo yatasaidia uwezekano
wa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo kwa nchi zote mbili.
Katika kikao kazi hicho Waziri Hasunga amemueleza Balozi huyo kuwa serikali ya
Tanzania imeanza zoezi la utambuzi wa wakulima nchini kwa kuwaandikisha ambapo
mpaka sasa wakulima wa zao la Tumbaku wamekwisha andikishwa.
Hasunga alisema kuwa lengo la zoezi hilo la
uandikishaji ni kuimarisha utambuzi wa wakulima ili serikali iweze
kuwahudumia kwa weledi wakulima kote nchini kupitia pembejeo mbalimbali za kilimo ili
kuondokana na wakulima hewa ambao wanatumia mwanya huo kuiibia serikali.
Vilevile amemueleza Balozi huyo kuwa serikali imejipanga kuimarisha sekta ya
utafiti wa kilimo nchini jambo litakaloongeza tija na manufaa makubwa kwa
wakulima nchini.
Katika mazungumzo hayo, Mhe Hasunga amemueleza Bi COOKE namna ambavyo serikali
ya Tanzania imejipanga kuimarisha masoko ya ndani na nje ya nchi kwa wakulima.
Bi. COOKE, kwa upande wake amefurahishwa na jinsi ambavyo Waziri wa
Kilimo pamoja na wasaidizi wake wanapambana kumsaidia Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kuimarisha sekta ya
kilimo sambamba na kuboresha masoko ya wakulima nchini.
Balozi huyo amemueleza waziri
wa kilimo kuwa Uingereza itaendeleza maradufu ushirikiano na Tanzania kwani ni
nchi yenye Amani na utulivu mwingi kwa wananchi wake.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment