
Maandalizi yote kwa michezo miwili ya kimataifa, yamekamilika.
Michezo hiyo ni kati ya Young Africans
ya Tanzania na Zanaco ya Zambia utakaochezwa Jumapili kuwania taji la
Ligi ya Mabingwa Afrika pia Azam FC ya Tanzania na Mbabane Swalows ya
Swaziland kuwania Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Kwa upande wa Young Africans dhidi ya
Zanaco, mchezo huo utafanyika Jumamosi Machi 11, mwaka huu. Waamuzi
kutoka Djibouti ndio watakaochezesha mechi hiyo.
Waamuzi hao ni Djamal Aden Abdi ambaye
atapuliza kipenga wakati wasaidizi wake ni Hassan Yacin na Farhan Salime
ilihali mwamuzi wa akiba atakuwa Souleiman Djamal. Kamisha katika
mchezo huo Na. 61 atakuwa Luleseged Asfaw kutoka Ethiopia.
Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu
wa Mratibu wa Mechi za Kimataifa wa Young Africans, Mike Mike ni Sh
20,000 kwa VIP ‘A’, Sh 10,000 kwa VIP ‘B’ na ‘C’ na Mzunguko (Viti vya
Rangi ya chungwa, kijani na bluu) ni Sh 3,000.
Azam wao watacheza Jumapili Machi 12,
mwaka huu na Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi, Dar es Salaam.
Waamuzi watakochezesha mchezo huo
wanatoka Benin ambao ni Mwamuzi wa kati, Addissa Abdul Ligali na
wasaidizi ni Medegnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina
huku Mwamuzi wa akiba akiwa Moumouni Kiagou na kamisha wa mchezo atakuwa
Mohamed Omar Yusud wa Kenya.
Kiingilio katika mchezo huo kwa mujibu
wa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba ni Sh 10,000 kwa VIP, Jukwa
Kuu itakuwa ni Sh 5,000 na Mzunguko itakuwa ni Sh 3,000.
Wakati huohuo, tiketi za waamuzi wa
Tanzania walioteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF),
kuchezesha mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya timu za AS Porto
Louis 2000 ya Mauritius na El Hilal ya Sudan wikiendi ijayo, wamepata
tiketi zao za kusafiri.
Katika mchezo huo ambao utafanyika ama
Machi 17, 18 au 19 Mwamuzi wa kati atakuwa Israel Mujuni Nkongo wakati
wasaidizi wake watakuwa ni Samuel Hudson Mpenzu na Josephat Deu Bulali
huku Mwamuzi wa akiba akiwa ni Hery Sasii. Kamisha katika mchezo huo Na.
78 atakuwa Jerome Kelvyn Damon kutoka Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment