Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela akizungumza na wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa.
Wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela (hayupo pichani).
· Mkoa wa Songwe umekuwa ukiongoza kitaifa hadi kufikia Desemba 2018 kwa kuwa na asilimia 76.4 ya kaya zilizojiunga na Mfuko wa Afya ya jamii uliopita (CHF) yaani kaya 198,376- Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Mafanikio hayo sharti yalindwe kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake ili pia tuongoze kitaifa katika Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (iCHF) - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· CHF iliyoboreshwa itakuwa na gharama juu kidogo yaani shilingi elfu 30 kwa kaya, tofauti na shilingi elfu 10 kwa kaya kwa mfuko uliopita, gharama hii bado itakuwa ni ndogo ukilinganisha na faida atakazopata mnufaika wa bima hii iliyoboreshwa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Mkoa kwa kushirikia na wadau wetu HIMSO umedhamiria kila kaya inakuwa mwanachama hai wa CHF iliyoboreshwa ili watu wenye kipato cha chini waweze kunufaika na huduma bora za Afya kama wanachama wengine wa Bima - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Natoa wito kwa halmashauri zote Mkoani Songwe kusimamia uandikishaji, kuhamasisha wanajamii na viongozi mbalimbali wajiunge na mfuko huu ulioboreshwa na pia kila halmashauri itenge fedha za kuyalipia makundi maalumu mfano wazee na Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Pia kila halmashauri zihakikishe kila Afisa Mwandikishaji ngazi ya kijiji au Mtaa anakuwa na simu, vituo vya kutolea huduma za Afya zinakuwa na simu na Kompyuta aidha watenge bajeti kwa ajili ya ajira za watumishi watakaoratibu zoezi hili - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Katibu Tawala Mkoa na timu ya watendaji wahakikishe vituo vyote vinatoa huduma bora kwa wanufaika wa mfuko wa CHF iliyoboreshwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha dawa, vitendanishi, vifaa na vifaa tiba vinapatikana - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Sitapenda kusikia mteja wa CHF iliyoboreshwa ananyanyapaliwa au kutengwa kwa namna yoyote ile katika kupatiwa huduma aidha nina wahimiza wadau wengine wa Afya kusaidia kuchangia kaya ambazo zitashindwa kujiunga kama vile wazee na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi - Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela
· Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Mdau wetu HIMSO umekamilisha maandalizi yote yanayohitajika kwa ajili ya kuanzisha mfuko mpya wa CHF iliyoboreshwa- Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.
· Mojawapo ya Shughuli zilizofanyika ni pamoja na kutoa Elimu kwa Viongozi mbalimbali ngazi ya Mkoa, Halmashauri, Wasimamizi ngazi ya kata 397 ( CHFs) na maafisa waandikishaji ngazi ya Kijiji/Mtaa (EOs) pamoja na ununuzi wa Vifaa vya uandikishaji uliofanywa na mdau wetu HIMSO - Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.
· Gharama za uchangiaji wa CHF iliyoboreshwa kwa kaya ni shilingi elfu 30 kwa kaya ya watu sita ambao kila mwanakaya ataweza kupata huduma za afya katika kituo chochote cha kutolea huduma ndani ya Mkoa Kuanzia ngazi ya Zahanati, Kituo cha Afya hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt Kheri Kagya.
· Naishukuru serikali na viongozi walionipatia kadi hii itanisaidia kupata matibabu bila kulipia kama ambavyo nilikuwa natakiwa kufanya hapo zamani, sasa nikienda hospitali nitaonyesha hii kadi kisha nitatibiwa – Oscar Kayange (Mtoto aliyepatiwa kadi ya iCHF wakati wa uzinduzi wa mfuko huo)
· Uzinduzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa Mkoa wa Songwe umefanyika Wilayani Songwe Mkwajuni ambapo viongozi na wadau mbalimbali walioshiriki wamechangia Zaidi ya shilingi milioni tisa katika harambee ya kusaidia kaya ambazo hazijiwezi ili waweze kujiunga na mfuko huo.
0 comments:
Post a Comment