Naibu
Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi.Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya
utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma kutoka kwa mwakilishi wa
Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Shogolo Msangi katikati wakati wa sherehe za
kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015
yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam na kushoto ni
Mwenyekiti wa NBAA Prof.Isaya Jairo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea
tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada ya kuwa
mshindi wa pili kutoka kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali
Bw.Shogolo Msangi kushoto wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa
wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya
jiji la Dar es salaam.
Afisa
Mkuu wa Mapato kutoka Kampuni ya kutengeneza Sementi ( Tanga Cement plc)
Bw.Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika tuzo ya washindi wa
jumla kwenye mashindano ya wawasilishi bora wa mapato kwa mwaka 2015.
Kwa
Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Shogolo Msangi katika waliokaa
wakati wa picha ya pamoja na washindi wa wawasilishaji bora wa mapato
wakati wa sherehe .
Picha Na Ally Daud-Maelezo.
Na Ally Daud-MAELEZO
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzoya utunzaji bora wa mahesabu kwa
taasisi za umma zilizoandaliwa na Bod ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa
mwaka 2015.
Akipokea
tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA), Bi. Anna Mndeme
alisema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu
ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya
uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).
“Tumefanya
vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na
kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana
na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na
Wahasibu (NBAA),” alisema Bi. Mndeme.
Aidha Bi.
Mndeme alisema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee
kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi
kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Bw. Richard
Kayombo alisema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi kwa
ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.
0 comments:
Post a Comment