Makamo wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akisoma
hotuba wakati wa uzinduzi wa mkutamo wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula
nchini (TAFOPA) uliofanyika juzi katika ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA), Susan Laizer
akisoma hotuba ya chama hicho iliyoelezea changamoto zinazowapata
wajasiliamali hao katika shughuli za uzalishaji na uuzaji wa bidhaa
zao.Mkutano huo umefanyika juzi katika ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo
Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
wajasiliamali wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA)
wakisikiliza kwa makini mafunzo yanayptolewa katika mkutano huo
uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo Jijini Dar es
Salaam.
Makamo wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu akiwa katika
picha ya pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles
Mwijage pamoja na baadhi ya wadau mbalimbali walioalikwa katika mkutamo
wa Chama cha Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA) uliofanyika juzi
kwenye ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kurekebisha Sera na Sheria
za kodi ili kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali kupata thamani
ya shughuli wanazozifanya.
Makamo wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu ametoa kauli
hiyo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Mkutano wa Chama cha
Wasindikaji wa Vyakula nchini (TAFOPA) uliofanyika katika ukumbi wa Mwl.
Nyerere uliopo Jijini humo.
Mama
Samia amesema kuwa wafanyabiashara na wajasiliamali nchini wamekuwa
wakilalamikia ongezeko la kodi katika bidhaa mbalimbali wanazozizalisha
hadi kupelekea kushindwa kuona faida ya shughuli hizo hivyo ni muhimu
kwa Serikali kusikiliza kilio chao kwa kutafuta namna bora itakayomaliza
tatizo hilo.
“Serikali
ya Awamu ya Tano imeliona tatizo hilo na imeahidi kulifanyia kazi kwa
kuzipitia upya sheria hizo na kuzifanyia marekebisho ili kila mwananchi
atoe kodi bila kinyongo na apate faida ya shughuli anayoifanya,”alisema
Mama Samia.
Amezitaja
changamoto zingine ambazo Serikali itazifanyia kazi ni kujenga
miundombinu katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wajasiliamali,
kupunguza muda wa upatikanaji wa leseni za biashara pamoja na
kuhakikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa inatenga maeneo kwa ajili ya
wajasiliamali hao.
Kwa
upande wake Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
amesema kuwa jambo analojivunia katika uongozi wake ni kuweza
kuwahamasisha Watanzania kuelewa ujenzi wa uchumi wa viwanda ambapo kwa
sasa nchi nzima wanazungumzia habari hiyo.
“Asilimia
kubwa ya wananchi wanazungumzia namna ya kuanzisha viwanda kama sehemu
ya kujipatia kipato na ndio maana mikutano ya wajasiliamali imekua
ikiongezeka siku hadi siku, hii inaonyesha dhahiri kuwa watanzania
wameamua kushirikiana na Serikali katika kuinua uchumi wa nchi kupitia
viwanda,”alisema Mwijage.
Naye
Mwenyekiti wa Chama cha TAFOPA, Susan Laizer amefafanua kuwa maeneo
yatakapotengwa yatasaidia kupunguza uharibifu wa mazao ya chakula
yanayovunwa wakati wa msimu husika pia yatatoa ajira nyingi kwa wananchi
watakaokuwa wakifanya shughuli za uzalishaji katika maeneo hayo.
“Tunaiomba
Serikali yetu itusaidie kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli zetu hadi
kwenye sehemu za vijiji ili wakulima wapate soko la bidhaa zao kwa
urahisi pamoja na kuepuka madalali wanaozorotesha vipato vyao,”alisema
Bi. Susan.
Aidha, Bi
Susan amempongeza Mama Samia kwa kuteuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa
mjumbe wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye jopo la
kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani ni sifa kwa Taifa na fursa kwa
wasindikaji wote nchini.
0 comments:
Post a Comment