Monday, December 5, 2016

TRA YASHINDA TUZO YA UTUNZAJI BORA WA MAHESABU KWA TAASISI ZA UMMA

tuzo
Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA) Bi.Anna Mndeme kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma kutoka kwa mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Shogolo Msangi katikati wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam na kushoto ni Mwenyekiti wa NBAA Prof.Isaya Jairo.
tuzo-1
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Rioba kulia akipokea tuzo ya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma baada ya kuwa mshindi wa pili kutoka kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Shogolo Msangi kushoto wakati wa sherehe za kukabidhi tuzo hizo kwa wawasilishaji bora wa mapato kwa mwaka 2015 yaliyofanyika nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
tuzo-2
Afisa Mkuu wa Mapato kutoka Kampuni ya kutengeneza Sementi ( Tanga Cement plc) Bw.Pieter De Jager wa pili kulia akiwa ameshika tuzo ya washindi wa jumla kwenye mashindano ya wawasilishi bora wa mapato kwa mwaka 2015.
Kwa Mwakilishi wa Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw.Shogolo Msangi katika waliokaa wakati wa picha ya pamoja na washindi wa wawasilishaji bora wa mapato wakati wa sherehe .
tuzo-3
Picha Na Ally Daud-Maelezo.

Na Ally Daud-MAELEZO

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshinda tuzoya utunzaji bora wa mahesabu kwa taasisi za umma zilizoandaliwa na Bod ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA) kwa mwaka 2015.

Akipokea tuzo hiyo Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Fedha (TRA), Bi. Anna Mndeme alisema kuwa wamepata tuzo hiyo kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA).

“Tumefanya vizuri na tumepata tuzo kwa kushika nafasi ya kwanza kutokana na kuwasilisha vizuri mahesabu ya mwaka wa fedha yaliyowasilishwa kufuatana na viwango vya uwasilishwaji vinavyozingatiwa na Bodi ya Ukaguzi na Wahasibu (NBAA),” alisema Bi. Mndeme.

Aidha Bi. Mndeme alisema kuwa tuzo hiyo ni chachu kwa TRA itayofanya waendelee kujituma zaidi katika ukusanyaji na utunzaji wa mapato ili kusaidia nchi kupata huduma bora za jamii kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Bw. Richard Kayombo alisema kuwa huo ni uthibitisho kwamba TRA inafanya kazi kwa ueledi na uwazi kupelekea kupata tuzo ya heshima.

Katika mashindano hayo Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) liliibuka washindi wa pili huku kampuni inayotengeneza saruji (Tanga Cement Plc) iliibuka kuwa washindi wa jumla kwenye tuzo hizo.

No comments:

Post a Comment