Mwanamazingira
Alexander Van der Bellen amepata ushindi katika duru ya pili ya
uchaguzi wa urais nchini Austria Jumapili hii Desemba 4, kwa mujibu wa
runinga ya taifa ya Austria. Amemshinda mgombea wa chama cha FPO,
Norbert Hofer, ambaye amekubali kwa haraka kushindwa kwake na kumpongeza
mshindani wake kwa "ushindi" wake.
Waangalizi
wamekua wakitarajia kukaribiana kwa wagombea hawa wawilii, kutokana na
jinsi uchaguzi wa duru ya kwanza wa mwezi Mei ulivyokuwa, ambapo
wagombea hao walishindana kwa kura chache kabla ya kura hizo kufutwa na
Mahakam ya Katiba.
Wapiga kura wa Austria wamekosoa utabiri uliokua umetolewa hapo awali.Alexander Van der Bellen, mwenye umri wa miaka 72, kulingana na matokeo mapya ni rais mpya wa Austria.
Kwa sasa anaongoza kwa 53.6% ya kura dhidi ya 46.4% alizopata mshindani wake, ambaye kwa haraka amekubali kushindwa.
"Nampongeza
Alexander Van der Bellen kwa ushindi wake na nawatolea wito wananchi wa
Austria kushikamana na kufanya kazi pamoja," amesema Norbert Hofer
ambaye amesema ana "masikitiko makubwa".
Alexander
Van der Bellen, ambaye aliwania katika mbio hizo za urais kama mgombea
binafsi, amepata kura nyingi katika maeneo mbalimbali ikilinganishwa na
kura alizopata katika duru ya kwanza mwezi Mei, ambazo zilifutwa na
Mahakama ya Katiba kutokana na kukiukwa kwa taratibu za zoezi la
kuhesabu kura.
Alexander Van der Bellen, amepata ushindi wa kura 31,000 dhidi ya msindani wake.RFI
0 comments:
Post a Comment