Na Mwamvua Mwinyi,Vigwaza
DIWANI wa
kata ya Vigwaza ,wilayani Bagamoyo mkoani Pwani,Muhsin Baruhan ametoa
msaada wa madawa ya magonjwa mbalimbali katika zahanati mbili ya Vigwaza
na Ruvu Darajani,yenye thamani ya mil.4.5.
Diwani
huyo ametoa madawa hayo kwa lengo la kupunguza makali ya uhaba wa madawa
unaokabili zahanati hizo na shirikiana na serikali kutatua changamoto
zinazokabili sekta ya afya.
Aidha
Baruhan ametoa msaada mwingine wa matofali 1,000 pamoja na mifuko ya
saruji 30 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba ya mganga mfawidhi wa
zahanati ya Ruvu Darajani .
Akikabidhi
misaada hiyo ,katika zahanati hizo,alisema ataendelea kutatua matatizo
yanayowakabili wakazi wa kata ya Vigwaza kwenye afya,maji,elimu na
kusaidia makundi maalum ikiwemo vijana,walemavu ,wanawake na wazee.
Alisema
fedha zilizotumika kununulia madawa ,mifuko ya saruji na matofali ni
nguvu yake mwenyewe na ni moja ya ahadi zake alizoahidi kuzitatua.
Baruhan
alieleza kuwa kwasasa watumishi wa afya katika zahanati hiyo wanaishi
katika nyumba za kupanga na kupata kero hasa nyakati za usiku kukitokea
mgonjwa wa dharura .
Aliomba wadau wa maendeleo,wa afya wajitokeze kushirikiana kujenga nyumba hiyo ili kuondoa kero ya kuishi mbali ya kituo kwenye nyumba za kupanga.
“Tulipiga
kelele sana kwenye baraza la madiwani kuhusu zahanati hii kuingizwa
katika mgao wa MSD ,tunashukuru mungu katusikia na sasa tumeingizwa
katika mgao wa madawa wa kusaidia na serikali”alisema Baruhan.
Baruhan alishukuru serikali na kuiomba ipeleke dawa kwenye zahanati kwa wakati ili wananchi wasihangaike .
Alimuomba
mganga mfawidhi katika zahanati ya Ruvu Darajani,afisa mtabibu zahanati
ya Vigwaza,kuyatunza madawa hayo kwani yanagharimu fedha nyingi.
“Kipindi
hiki ni kigumu kiuchumi, dawa hizi zitumike vizuri,ningeweza kuanzisha
duka la vipodozi ama la madawa lakini nimeona umuhimu wa kushirikiana na
jamii ambayo ilinijali kwa kunichagua ili iweze kunufaika na kuondokana
na kero ya kununua madawa kwenye maduka ya nje ya vituo”alisema.
Nae
mganga mfawidhi wa zahanati ya Ruvu Darajani,Gilbert Mkotigwa,alisema
zahanati hiyo ilikuwa haijaingizwa katika mgao wa dawa kutoka bohari ya
madawa (MSD)kwa miaka mitatu iliyopita tangu feb 2014 hadi sept 5 mwaka
huu.
Alisema
katika kipindi hicho walikuwa wakisaidiwa na zahanati za jirani ikiwemo
Visezi,Kidogozero,Milo,Vigwaza pamoja na wilaya ambayo ilikuwa ikitupa
mgao kutokana na fedha za OC.
Dk,Mkotigwa alisema kutokana na uhaba huo ndio uliomsukuma diwani kuomba orodha ya madawa wanayoyahitaji ambapo amewasaidia.
Alisema licha ya kupokea msaada huo lakini bado zahanati inakabiliwa na matatizo mengine ikiwa ni sanjali na ukosefu wa nyumba ya mganga na watumishi,wodi ya uzazi kwani kwa sasa wanaojifungua wanajifungulia katika chumba kidogo ,mashine za kupimia wingi wa damu,sukari na haja kubwa.
Changamoto
nyingine ni ukosefu wa chumba cha maabara,wazee wa kijiji kutoingizwa
katika mpango wa mfuko wa kusaidia wazee na kaya maskini(TASAF).
Dk.Mkotigwa
alisema kukosekana kwa mashine ya kupimia wingi wa damu kunasababisha
wajawazito kwenda kupima wingi wa damu kituo cha afya Mlandizi ambayo
imekuwa kero kwa wajawazito kufuata huduma hiyo mbali huku ikiwa ni
kipimo muhimu kwao tangu kushika mimba hadi kujifungua.
Alimuomba
diwani huyo kushirikiana na wahisani wengine kuangalia namna ya
kusaidia upatikanaji wa vipimo hivyo na kutafutia ufumbuzi changamoto
hizo ili kutoa huduma bora .
Alisema zahanati hiyo inahudumia wagonjwa wa ndani na nje 400-500 kwa mwezi na wajawazito 10 hadi 15 katika kipindi hicho.
Afisa tabibu wa zahanati ya Vigwaza ,Alexander Ngalawa ,alisema zahanati hiyo ina hudumia vijiji vitano na ipo karibu na barabara kuu ya Morogoro-Dar-es salaam hivyo watu wengi kukimbilia kupata huduma ya afya.
Alisema
bado wana upungufu wa madawa ,unaotokana na kupelekewa upungufu wa
madawa wanayooda kupitia wilaya kwenda bohari na kusababisha upungufu
katika mahitaji yao.
Dk.Ngalawa
alieleza kwenye zahanati hiyo wapo watumishi watatu ambao hawatoshi
,mmoja akipata likizo wanabaki wawili hivyo kuhemewa na wagonjwa .
Alimshukuru diwani wa kata ya Vigwaza kwa kutoa msaada wa madawa na kuahidi kuzitumia vizuri kwa utaratibu unaotakiwa .
Mkazi wa kijiji cha Vigwaza Zulfa Hassan alisema madawa hayo yatasaidia hasa watoto ,wazee na akina mama .
0 comments:
Post a Comment