Mgombea
kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani,
Donald Trump, amemshutumu mpinzani wake Bi Hillary Clinton kwa kutumia
aina fulani ya dawa, wakati wa mjadala wao uliopita wa moja kwa moja wa
runinga.
Anasema kuwa alikuwa na haiba mwanzo mwanzo wa mjadala huo.
Sasa
anapendekeza kuwa wafanyiwe majaribio ya matumizi ya dawa, kabla ya
kufanyika kwa mjadala wao wa mwisho hapo siku ya Jumatano ya wiki hii.
Katika
mkutano wake wa hivi punde uliofanyika New Hampshire, Bwana Trump kwa
mara nyingine, amedai kuwa kuna njama za kumuibia kura.
Timu ya
kampeini ya Bi Clinton, imesema kwamba wapigaji kura, sasa wameona
bayana kile anachokiita juhudi za aibu za Bwana Trump za kutaka kuhujumu
shughuli za upigaji kura.
0 comments:
Post a Comment