HOTUBA
YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA ISIMANI KWA TIKETI YA CHAMA
CHA MAPINDUZI MWAKA 2015
UTANGULIZI
UTAMBULISHO
Jina
langu naitwa FESTO FUNGAMEZA KISWAGA. Nilizaliwa mwaka 1974 katika kijiji cha
malinzanga, kata ya Mlowa ,Tarafa ya idodi ,Wilaya ya Iringa vijijini, Mkoa wa
Iringa. Mimi ni mtoto wa nne katika familia ya watoto watano katika familia ya
Mzee Fungameza Kiswaga. Mzee Kiswaga alikuwa Mkulima wa Kawaida katika Kijiji
cha Malinzanga ,kata ya Mlowa ,wilaya ya Iringa Vijijini.
TAALUMA
·
Shahada
(Degree) ya sayansi ya usimamizi wa wanyamapori kutoka chuo Kikuu cha
Dar-es-salaam (2007-2010)
·
Diploma
ya usimamizi wa Maliasili Chuo kikuu cha maliasili, Mweka, Moshi (2001-2003)
·
Elimu
ya sekondari Mkwawa high school (1993-1995)
·
Elimu
ya Sekondari (1989-1992) Malangali sec school
·
Elimu
ya Msingi (1982-1988) shule ya msingi Mlowa Iringa vijijini.
MAFUNZO
MBALIMBALI
·
Kozi
ya usimamizi wa shughuli za maendeleo kwa nchi zinazoendelea ; Nanchang,
Shanghai na Beijing –China (2014)
·
Kozi
ya namna ya tathimini maendeleo ya watu katika nchi za afrika Tripoli,Libya
(2010)
·
Kozi
ya masuala ya usimamizi rasilimali na usalama maeneo ya mipakani, Nairobi-KENYA
(2007)
·
Kozi
ya mafunzo ya uendeshaji wa bima ya afya ,Mtwara (june,2014)
·
Kozi
usimamizi wa mipaka ya nchi na ulinzi wake, Nairobi (july,2006)
·
Kozi
ya ufuatiliaji ya uboreshaji wa shughuli za kilimo , Manyara (May, 2005)
·
Mafunzo
ya juu ya uongozi na kuzuia ugaidi Kutoka Max International Security academy,
Tel viv, Israel (2007)
·
Mafunzo
ya kozi ya kutunga sera na kuondoa umasikini
Arusha,2014
·
Kozi
ya uendeshaji mashirika makubwa (Novotel hotel, 2004)
·
Kozi
ya uongozi na itikadi ya chama, 2009 (Makao makuu ya Chama -Dodoma)
·
Kozi
ya viongozi wakuu wa serikali za Wanafunzi wa vyuo vikuu wa afrika mashariki,
2010 Kigali-Rwanda.
·
Kozi
mbalimbali za usimamizi wa rasilimali na ulinzi wa watu.
UZOEFU
WA UONGOZI
Ndugu zangu wana isimani mimi
nina uzoefu wa wa uongozi kama ifuatavyo;-
· May 2015 mpaka ninavyoongea
sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi,Bukoba –mkoa wa Kagera
· Feb –May 2015 Mkuu wa wilaya
Mvomero, Morogoro
· May 2012-Feb 2015 Mkuu wa
Wilaya ya Nanyumbu,Mkoa wa Mtwara.
· 2005-2012- Mkuu wa Idara ya
Ulinzi na Usalama Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) –Hifadhi ya
Serengeti,Mkoani Mara.
· 2007-2008- Nilichaguliwa kuwa
Mbunge wa Bunge la Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam. Baada ya
kufanya vizuri katika kuwawakilisha wanafunzi wenzangu mwaka 2009-2010
nilichaguliwa kuwa Rais wa wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar-es-salaam (DARUSO)
· 2009-2010-Mjumbe wa bodi ya
wakurugenzi, Katika Chuo kikuu cha Dar-es-salaam (UDSM)
· 2009-2011-Nilichaguliwa kuwa
Rais wa umoja wa shirikisho la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki ambapo
inashirikisha zaidi ya vyuo 400 vya elimu ya juu katika nchi za Tanania,Kenya,Uganda,
Rwanda na Burundi. Ushindi huu wa kuwa niliupata katika mkutano uliofanyika
July 2009 mjini Nairobi, nchini Kenya- Ulikuwa ni ushindi wa heshima kwa nchi
yetu Tanzania kwani wagombea walikuwa watano kutoka nchi zote na mimi
nilichaguliwa kwa kishindo ambapo nilipata asilimia 76 ya kura zote.
· 2001-2003-Makamu wa Rais wa
serikali ya Wanataaluma wa chuo kikuu cha Kimataifa cha Wanyamapori,Mweka
–Moshi,Kilimanjaro. Wakati huo huo 2001-2003-Mjumbe wa Bodi Chuo kikuu cha
Wanyamapori-Mweka,Moshi –Kilimanjaro.
· 2003-2005-Mkuu wa kanda katika
Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mkoa wa Iringa.
· 1996-2001- Mwenyekiti wa Mradi
wa MBOMIPA, mradi ambao unashirikisha vijiji 21 katika Tarafa za Idodi na
Pawaga- Nafasi ilionisaidia kufahamu vizuri tarafa za Pawaga na Idodi hasa
katika eneo la changamoto na fursa za vijiji vyote 21 vya eneo hili la mradi.
· Nilishawahi kushika nafasi
nyingine mbalimbali katika kampuni za uwindaji wa kitalii na taasisi zingine.
· 2012- 2015-Katibu wa Wakuu wa
Wilaya ya Mtwara, pia Mwenyekiti wa Wakuu wa Wilaya ya Morogoro Feb 2015.
· Kozi ya maendeleo ya binadamu
katika ulimwengu wa Anuwai, UNDP, 2009 Nairobi, Kenya.
TUNZO NILIZOWAHI KUTUNUKIWA
· Tunzo ya uongozi uliotukuka
kutoka chuo Kikuu cha Dar-es-salaam
· Tunzo ya uongozi uliotukuka
kutoka chuo kikuu cha wanyamapori ,Mweka Moshi.
· Tunzo ya uongozi kutoka taasisi
inaojishughulisha na Elimu katika vyuo vikuu vya Africa mashariki.
· Hati iliotukuka kutoka chuo cha
mafunzo ya ulinzi wa raia- Insitute of terrorism research and response, Israel.
· Cheti cha usimamizi uliotukuka katika
mkutano wa dunia wa kujadili maendeleo duniani; kutoka taasisi ya World
Economic Forum, uliofanyika-Dar-es-salaam, Tanzania 2010.
UONGOZI KATIKA CHAMA
· 2012 mpaka sasa ;Mjumbe wa
kamati ya siasa CCM wilaya (kwa cheo
changu)
· 2012 mpaka sasa; Mjumbe wa
halmashauri kuu mkoa kupitia kata ya Mlowa
· 2007-2012 Mjumbe wa halmashauri
kuu CCM wilaya ya Iringa vijijini (wajumbe 10 wa kuchaguliwa na mkutano mkuu).
· Mwenyekiti wa kamati ya vijana
wa CCM katika mkutano wa semina ya viongozi vijana wa CCM 2010; Dodoma.
HISTORIA
YA JIMBO LA ISIMANI
Jimbo
la Isimani lipo katika Wilaya ya Iringa, Jimbo hili lina tarafa 3 yaani
Isimani, Pawaga na Idodi. Jimbo hili lina Kata kumi na tatu; ambazo ni
Kising’a, Kihorogota, Malengamakali, Nyang’oro,Izazi na Migoli. Zingine ni
Mboliboli (kata Mpya), Itunundu, Mlenge,ilolompya, Mlowa,idodi na Mahuninga.
Jimbo
hili linabeba jina maarufu katika maendeleo ya Tanzania kwani isimani katika
miaka ya sitini mpaka themanini mwanzoni isimani ilisifika kwa kilimo cha zao
maarufu ya chakula zao la mahindi. Hii ndio ilipelekea Hayati Mwalimu Nyerere
kujenga Ghala la Taifa la Chakula Mkaoni Iringa ghala ambalo lipo mpaka leo
japo harihifadhi mahindi ya kutoka isimani tena kwa sababu ya kuporomoka kwa kilimo
hiki kwa sababu mbalimbali. Kwa ujumla wake jimbo la ismani kwa maana isimani
yenyewe,pawaga na Idodi tarafa zote zimejaliwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo
hazijaendelezwa na kuwekewa mikakati ambayo itasaidia kuinua hali ya maisha ya
sisi wananchi tunaoishi katika jimbo. Hata hivyo Jimbo hili ambalo linabebwa
zaidi na maendeleo ambao ni ya kitaifa na hivyo kuwa ni moja ya jimbo
yanayotegemea mipango ya mpito (yaani maendeleo ambao ni mipango unganishi ya
Mikoa na Wilaya zingine); Mfano Jimbo hili lipo katika njia kuu ya Mbeya kwenda
Arusha kupitia Dodoma hivyo kujikuta barabara kuu hii ambao katika serikali ya
awamu ya nne chini ya Rais wa Jamhuri Muungano Dr Jakaya Mrisho Kikwete
ameijenga kwa Kiwango cha Lami (barabara hii inatoka iringa Mjini kupitia eneo
la jimbo la isimani,eneo la jimbo la mtera,Dodoma mpaka Arusha. Bahati nyingine
ni kwamba barabara nyingine inatoka iringa Mjini kuelekea hifadhi ya Taifa ya
Ruaha
Kwa
upande wa miundombinu ya barabara a halmashauri mkurugenzi wa Halmashauri
amekuwa anajitahidi sana kuhakikisha barabara hizi zinapitika muda wote katika
kipindi chote cha mwaka. Hata hivyo ipo changamoto kubwa kwa baadhi ya vijiji
kutounganishwa na mtandao wa barabara katika eneo kubwa la jimbo.
HALI
YA SASA KIUCHUMI NA MAENDELEO YA WATU
Ukiachilia
mbali suala la barabara jimbo la isimani kwa ujumla liko katika hali mbaya
kiuchumi; Tarafa ya Isimani ambao jamii katika kata za kising’a, kihorogota, malengamakali,
na nyangoro asilimia 100 zinategemea kilimo na ufugaji; ilitegemea kilimo
imekuwa inaporomoka kiuchumi mwaka hadi mwaka, hali ni si nzuri na ikiachwa
namna ni hatari na haivumiliki. Kwa sababu in madhara makubwa sana katika
maendeleo ya jamii husika. Pamoja na tatizo la mvua kuwa chache lakini
umekosekana ushirikishwaji wa jamii husika yaani pengo kubwa na wananchi hawa
pamoja na ari kuwa walionao ya kujiletea maendeleo kimekosekana kiungo muhimu
sana kati ya wananchi na taasisi za utafiti wa kilimo ambapo katika maeneo
mengine amabao yapo na hali ya kama ya isimani uzalishaji wa mazao umekuwa
unapanda mwaka hadi mwaka. Kwa nini isimani tu?
. Jamii za kata za Izazi na Migoli na wakulima,wafugaji na uvuvi jamii ya eneo
hili nazo kiuchumi inazidi kushuka tena kwa kiwango cha kutisha, jamii za maeneo haya uchumi wao unashuka kwa
sababu ya kukosa msaada ya ushauri mbinu za kilimo, uvuvi na ufugaji, katika
eneo hili katika kipindi cha miaka thelathini wananchi hawajawahi kupata
msukumo wa ni namna gani wanaweza kurudi katika uchumi waliowahi kumiliki miaka
ya nyuma wamebaki bila matuamini yoyote
Ni
lazima hali hii inatafutiwa mikakati ya kukabili haraka sana kwani tayari
imeshaleta athari kubwa kiuchumi na kijamii katika tarafa hii iliosheheni
udongo wenye rutuba sana na yenye jina kubwa.
Tarafa
ya pawaga ambao kwa uhakika ina hazina ya ardhi yenye rutuba na miundombinu ya
umwagiliaji, asilimia kubwa ya jamii inajitegemea katika kuhakikisha miundombinu
hiyo inafanyakazi. Utegemezi huu unarudisha nyuma jitihada na uchapakazi wa
jamii hii. Pamoja na tarafa hii kuwa na bahati ya kuwa katika eneo hili bado
kipato katika kilimo cha mpunga hakina record nzuri ya kupanda kwa sababu ya
kukosa mikopo kwa wakulima wadogo ili kuwawezesha kuingia katika ukulima wakati
na mkubwa kama ilivyo katika mabonde mengine ya Dakawa-morogoro, kilombero na
mbarari. Hii imedumaza sana uchumi wa wananchi wa
Pawaga. Jitihada kubwa inaotumika na wakulima hao inahitaji
msaada wa kuwasukuma ili waweze kwenda mbele kwa kasi zaidi kwa vile kila kitu
wanacho hili lazima lishughulikiwe sasa na sio baadae. Wafugaji wa eneo lote la
jimbo la ismani hawajawahi kushirikishwa katika kuwatambua na kuwapa misukumo
ili nao wachangie pato la jimbo kwa sababu wameachwa kila mfugaji anahaingaika
na mifugo yake hii haikubariki hata kidogo.
Eneo la kubwa la tarafa inapakana na hifadhi
ya Taifa ya Ruaha na pia pori tengefu la Lunda Mkwambi. Pamoja na hali hii
wananchi wamekuwa hawafaidi chochote kutoka katika eneo hili bali wamekuwa
wanapata adha kubwa na wanyamapori waharibifu kama tembo na wanyama wengine.
Kibaya zaidi kuna mradi wa MBOMIPA ambao ndio lnapaswa kuwa mukombozi wa vijiji
hivi lakini matokeo yake mradi huu umekuwa unamilikiwa na watu wachache na
wananchi hawashirikishwi tena kama inavyopaswa kuwa. Ikumbukwe wakati mradi huu
unaanzishwa wananchi walishirikiswa lakini sasa umekuwa wa wachache na wananchi wamekosa
imani na wasimamizi wa mradi huu maana sio wao tena.
Tarafa
ya Idodi, ni tarafa ambayo ina rutuba ya kutosha kwa kilimo na ndio tegemeo
kubwa la jamii ya eneo hili. Kama ilivyo isimani jamii na wananchi tumekosa
matumaini ya kilimo kwa sababu ya kukata tamaa. Miundombinu ya umwagiliaji
hakuna wakati upo uwezekano wa kuweka upo.
Katika kata ya mlowa ahadi za kujengewa kwa muundombinu huu imekuwa ya muda
mrefu na mpaka sasa haijakamilika.
Eneo
la Idodi kuna changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji, wanyama
waharibifu na uchumi uliodumaa. Kumekosekana na ushauri wa kuondokana na hali
ya umasikini ambao unaendelea kushamiri katika
tarafa hii. Kazi nzito
inafanywa na wananchi katika kujiletea maendeleo inaishia katika kuhangaika na
kilimo kisicho na kipato cha maana. Kwa tafsiri ni lazima mfumo na namna ya kushughulikia
uchumi wa tarafa hii uanze mara moja bila kuchelewa.
CHANGAMOTO ZILIZOPO
Ni jukumu la kiongozi yeyote makini anapotaka
kugombea uongozi katika ngazi mbalimbali kujua changamoto na kuibua fursa
zinazopatikana katika ndani na nje ya eneo husika ili kuhakikisha wananchi
wanapata unafuu wa maisha na pia kujielewa muskabali wao na watoto wetu. Hata
hivyo changamoto nyingi sana katika jimbo hili zimekosa kiongozi mwenye uchungu
kami mimi.
Katika tafakari hiyo jimbo la isimani
linakabiliwa na tatizo la maji. Ikumbukwe kuwa jimbo hili linapitiwa na mto
Ruaha mdogo katikati, mto huu hutiririsha maji mwaka mzima. Pia jimbo hili kwa
upande wa magharibi kuna bwawa kubwa la mtera ambalo pia hukaa mwaka mzima wa
mwaka. Lakini jimbo hili asilimia 70 lipo uwanda wa chini ambao ni rahisi
kushughulikia maji kwa gharama nafuu kwa maji kusambazwa kwa mtiririko
(gravity) pamoja na kuwa na bahati hiyo kuna tatizo kubwa sana la maji.
Kwa ujumla tangu jimbo hili lizaliwe miaka
zaidi ya ishirini iliyopita tatizo la maji halijashughulikiwa kwa kiwango cha
kuridhisha. Nikipata ridhaa ya CCM na Hatimaye kuteuliwa kuwa Mbunge
nitahakikisha njaa inabakia historia ili wananchi waungane na wenzao majimbo
mengine wanaofurahi hali bora ya huduma za jamii na hasa maji.
HALI YA MAJI JIMBONI
Serikali yetu imetekeleza miradi mbalimbali
katika azima ya kusogeza huduma za maji jirani na wananchi. Miradi ya maji
kupitia benki ya dunia, na pia za Sweden.
Kuna jitihada zimefanyika kupitia wadau wa
maendeleo yaani Familia ya Huwel hususani mr sarehe na Ahmed. Kuna kazi nzuri
imefanywa na kanisa Katoliki na pia kanisa la anglikana; wadau hawa wa
maendeleo ninawapongeza sana kwa kazi nzuri.
Hata hivyo jimbo hili bado lina shida kubwa
sana la maji ya kunywa na kwa ajili ya mifugo na matumizi mengine. Ahadi nyingi
za wananchi kutupatia maji nyingi zimedumu miaka mingi na hazina dalili za
kukamilishwa. Kwa hiyo zinahitaji msukumo mpya na mtu pekee anayeweza kukabiliana
matatizo haya ni mimi.
Sisi wananchi wa Isimani kwa umoja wetu
tunaweza, tunaweza. Mipango ya namna ya kukabilna na suala hili nitaliekeza
wakati wa kampeni zangu kuanzia tarehe 20 july 2015.
KILIMO
Kama nilivyoeleza hapo juu sekta ya kilimo
katika jimbo la isimani imekufa, sekta hii imekufa kwa sababu ya kukosekana kwa
mbinu mbadala za kuendeleza kilimo. Matokeo yake tunaaminishwa kuwa tutaletewa
chakula cha msaada; sisi wananchi wa isimani tutajipanga kurudisha heshima yetu
kwa kurudisha kilimo cha kisasa na mbegu za kisasa zitatafutwa kokote ziliko
ili ziwe isimani. Kazi hii haijafika toka miaka thelathini iliyopita . mipango
yangu nitaiweka hadharani wakati wa kampeni.
Njaa katika jimbo hili inataka kuzoeleka kama
vile ni jambo zuri. Nikipata ridhaa ya CCM na Hatimaye kuteuliwa kuwa Mbunge
nitahakikisha njaa inabakia historia ili wananchi waungane na wenzao majimbo
mengine wanaofurahi hali bora ya chakula.
BARABARA
· Halmashauri
ya wilaya ya iringa imejitahidi kufanya matengenezo kwa barabara lakini zipo
barabara muhimu ambazo hazijafunguliwa ili kufufua uchumi na mawasilaiano
miongoni mwa wana ismani.
AFYA
· Huduma
za afya bado katika vijiji na maeneo bado haziridhishi, mipango yangu katika
eneo hili nitazileza katika kampeni zangu.
ELIMU
· Kuna
vijana wengi wamemaliza form four na vyuo vikuu wapo vijijini. Nitaeleza
mipango wakati wa kampeni zangu.
UMEME
· Naomba
nimshukuru DR Jakaya Mrisho Kikwete kwa kazi nzuri ya kupeleka umeme vijijini
ambapo vijiji zaidi ya 3000 nchi nzima ambapo kupitia REA viijiji vinawaka.
Hata hivyo kumekuwepo na upendeleo kwa baadhi ya vijiji hawajapata na vitongoji
katika vijiji vingi bado haujapelekwa. Majibu ya suala hili yamekuwa ya
kukatisha tama
HITIMISHO
Jimbo
hili lina fursa nyingi ambazo kwa makusudi au kwa bahati mbaya hazijatumika kwa
malengo maalumu. Ninaomba leo niwajulishe wanaisimani kuwa muda utakapofika
nitachukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la isimani. Fursa hii ni muhimu sana
kwa wanaisimani wenzangu ambao wamevumilia kwa kipindi kirefu shida wanazokabilina
nazo ambazo sasa zitapata uvumbuzi kupitia kwangu endapo wanaismani mtanipa
ridhaa ya kuwatumikia.
Festo
kiswaga
Mtangaza
nia pia ni Dc msenyi-mkoani
Kagera.
0 comments:
Post a Comment