Mkurugenzi mtendaji TFRA Dkt. Stephen Ngailo. akiwa katika picha na Matlida Kasanga afisa mawasiliano na mahusiano wa TFRA na ofisa udhibiti ubora Cothal Samwel Kwenye mafunzo ya matumizi sahihi ya mbolea ukumbi wa Halmashauri ya Ikungi Singida.
Na Hamis Hussein - Singida
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA imewataka wakulima kila mmoja kuwa balozi katika kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo ili kuongeza tija kwao binafsi na taifa kwa ujumla .
zaidi ya wakulima 200 kutoka halmashauri ya ikungi wameshiriki mafunzo ya matumizi ya mbolea yaliyoratibiwa na TFRA ambapo mikoa ya Singida , Dodoma na Tabora imepewa kipaumbele kwa kuwa ndio wazalishaji wakuu wa zao la alizeti .
Akizungumza katika mafunzo yao mkurugenzi Mtendaji wa TFRA Dkt. Stephen Ngailo amesema wao kama mamlaka ya udhibiti wa mbolea kwa kushirikia na wizara ya kilimo na wadau wengine kwa ujumla lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuona mnufaika mwa mwisho wa mbolea aidha muuzaji au mkulima apate tija kulinga na mbolea hiyo ili kuongeza uzalishaji .
"Tunatoa sahihi kwa wakulima, afisa kilimo na wadau wengine kama vile wauzaji wa pembejeo kuhakikisha ile elimu iwasaidie kutumia mbolea kwa usahihi , lengo ni kuwa wewe unayetumia mbolea shambani unapata faida , kuwe na tofauti ya tija kwa wewe ulieweka mbole, kuonyesha kuwa kuweka mbolea inalipa ". alisema Dkt. Ngailo
Dkt. Ngailo ametumia nafasi hiyo kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora za kilimo ikiwa ni lengo la serikali katika mkakati wake wa kuhakikisha zao la alizeti linazalishwa kwa wingi ili kupunguza uagizaji wa mafuta toka nje ambapo mikoa ya kimkakati ni singida , dodoma na Tabora.
"Mheshimiwa waziri mkuu alikuja singida kuhamisisha mkakati kuuu ikiwa nia adhma ya kuongeza wa zao la alizeti ili kujitoshereza katika uzalishaji wa mafuta . kuna mikoa ya kimkakati , Kuna mkoa wa dodoma niwashuruku wataalamu wetu wametoa mafunzo kama haya , mkoa wa singida na baadaye ni igunga mkoa wa Tabora na haya ndio maeneo yalichaguliwa kuwa ndio wazilishaji wakuu wa zao la alizeti" . Ameongeza Dkt. Ngailo.
Kaimu mkuu wa idara ya kilimo ushirika na umwagiliaji kutoka halimshauri ya Ikungi Mkoani singida Gurisha Msemo amesema hali halisi ya matumizi ya mbolea katika halmashauri hiyo bado ipo chini kwa mpaka sasa 5% ya wakulima ndio wanautumia mbolea ya chumvichumvi.
" Matumizi ya mbolea katika halmashauri ya ikungi ni 5 % asilimia nyingine wanatumia samadi lakini pia kuna familia au wakulima hawatumii kabisa mbolea kwa hiyo sasa baada ya mafunzo haya tunatumaini watakuwa wamepata elimu ya juu ya matumizi ya mbolea". alisema Gurisha
Baadhi ta washiriki wa washa hiyo ilikusudia kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea na kanuni bora zakilimo wamesema dhana potofu iliyopo mtaani ya kuamini kuwa mbolea ya chumvi chumvi inaharibu ardhi ndio sababu kuu ambayo ilikuwa inapelekea wao kutotumia mbolea katika mashamba yao .
Halmashauri ya Ikungi inatarajia kuzalisha tani 72000 za alizeti kutoka kwa wakulima 95000 na kupitia mafunzo hayo tija ya mkulima mmoja mmoja kama atazingatia kanuni bora za kilimo kama ambavyo mamlaka ya udhibiti wa mbolea nchini TFRA kiwago za uzalishaji wa mafuta kitakuwa juu sana.
0 comments:
Post a Comment