Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji mradi wa maji Imalabupina-Ichwankima wilayani Chato. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Geita.
Kulia ni Mhandisi wa Maji wilayani Chato akitoa ufafanuzi wa mradi huo kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.

Mbunge wa Viti Maalum mkoani Geita, Vicky Kamata akisalimia wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi mradi wa maji Imalabupina-Ichwankima.
Mapema asubuhi kwenye mapokezi ya Mhe. Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Chato
Burudani ya asili kutoka kikundi cha Bugobogobo

Na George Binagi, GB PazzoWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa maji Imalabupina-Ichwankima uliopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
Mhe. Majaliwa ambaye jana alianza ziara ya kikazi mkoani Geita, alisema utaondoa kero ya maji kwa kwa wakazi wa wilaya ya Chato ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa serikali wa kumtua mama ndoo kichwani na hivyo kumtaka Mhandisi wa Maji wilayani humo kuhakikisha mkandarasi anamaliza mradi huo kwa wakati.
Mhandisi wa Maji wilayani Chato, alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi Februari na kuwahudumia wakazi wa Vijiji 11 ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi Bilioni 8.2.

Tazama Video hapa chini
0 comments:
Post a Comment