Makarani wa sensa wakipokea mafunzo ya sensa yanayoendelea mkoani singida
Mratibu wa sensa ngazi ya mkoa wa Singida Ndugu Naing'oya Kipuyo akikagua makarani wa sensa wanavyopewa mafunzo hapo jana katika shule ya Msingi Mramba Mafunzo ya makarani wa sensa mkoa wa Singida Yakiendelea Mwalimu Filbert Limo msimamizi wa maudhui ya sensa mkoa singida akizungumzia mafunzo hayo.
![]() |
Mafunzo yakiendelea |
![]() |
Mafunzo yakiendelea |
![]() |
Rukia Swido Mwenyekiti wa makarani katika kituo cha ilongero akizungumza katika mafunzo hayo |
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Sensa Mkoa wa Singida Naing’oya Kipuyo alipotembelea maeneo ya Wilaya ya Singida vijijini na Manisapa ambapo mafunzo hayo yanaendelea huku akiwasisitizia kwamba watakaoshindwa katika mitihani yao hawataendelea na mafunzo kwa kuwa Serikali inataka Watumishi watakaoweza kuleta matokeo yaliyotarajiwa.
Kipuyo amesema mafunzo hayo yatahusisha watendaji wa Kata Makarani, Maafisa Tehema, Wasimamizi wa maudhui ambayo yatadumu kwa muda wa siku 19 huku Watendaji wa Kata wapatao 139 Mkoa mzima watapata mafunzo hayo kwa muda wa siku mbili tu kuanzia tarehe 31 Julai 2022 mpaka tarehe 1 Agosti 2022 ili waweze kuendelea na zoezi la uhamasishaji katika maeneo yao.
Hata hivyo amepongeza utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa mafunzo ya namna ya kukamilisha zoezi hilo ambapo amebainisha kwamba katika mkoa wa Singida kuna vituo 22 vya kutolea mafunzo ambapo vyote hakuna changamoto iliyojitokeza.
“Sisi kama wasimamizi wa ngazi ya mkoa tunaamini zoezi hili litafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu tunao Makarani wenye uwezo mkubwa kutokana na namna walivyopatikana kupitia sifa na vigezo mbalimbali vilivyotumika kuwapata” alisema Kipuyo.
Bwana Kipuyo alieleza kwamba mkoa wa Singida una jumla ya Madarasa 28 ambako mafunzo yanaendele na jumla ya makarani 5449 ambao watapatikana kupitia wakufuzi walipata mafunzo ngazi ya pili ya mkoa.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu shule ya msingi Mramba Rukia Swido ambaye pia ni Mwenyekiti wa Makarani katika kituo cha Ilongero amesema ili waweze kufanikiwa Makarani wanaaswa kuwa na haiba ya uvaaji ili waweze kukubalika katika jamii watakayokuwa wakiihesabu kwa kuwa uvaaji huweza kusababisha mtu kupokelewa vibaya katika jamii.
Mwalimu Rukia aliendelea kufafanua kwamba wakimaliza mafunzo hayo watashuka ngazi za chini mpaka kufikia kwenye vitongoji ambapo watatumia lugha nzuri na yenye ushawisha pamoja na kuwahakikishia wateja wao kwamba taarifa hizo zitabaki kuwa siri baina ya Karani na mhojiwa.
Elizabeth Ramadhani ni Mtendaji ni wa Kata ya Ntonge ameishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kutoa semina ya siku mbili ambayo ameeleza kwamba itawasaidia katika kuendesha majukumu yao ya uhamasishaji kwa jamii kuhusu zoezi hilo.
Ameeleza kwamba watafanya jukumu hilo kwa ufasaha na kwamba habari watazifikisha katika kamati zote za sensa pamoja na vikao mbalimbali kama sehemu ya kuhamasisha ushiriki wa kila mwananchi katika zoezi hilo.
Kuhusu usimamizi wa maudhui mwalimu Filibert Salvatory Limo kutoka shule ya Ikanoda alisema wakufunzi wamewafundisha miongozo mbalimbali ambayo imewapatia mwanga mkubwa na wameweza kutambua namna ya kuendesha na kusimamia zoezi kwa weledi ili kuandika historia mpya ya nchi yetu.
Naye Mtendaji wa Kata ya Mungumaji Bakari Ntandu amesema mafunzo ya siku mbili waliyoyapata yamekuwa chahu kwao katika kuimarisha uhamasishaji kwenye vijiji na vitogoji wanakofanya kazi huku akiendelea kuiomba Serikali kuendela kukutana na makundi maalum kama boda boda jambo ambalo litasaidia kuongeza uelewa wa wananchi.
0 comments:
Post a Comment