Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imeombwa kuchukua hatua dhidi ya
Kalomba online TV ambayo imekuwa na mwenendo mbaya wa kuchafua viongozi na
kuwasingizia kifo na hivyo kuzusha
taharuki kwa jamii.
TV hiyo ya mtandao mwishoni mwa wiki iliyopita ilimzushia kifo Waziri wa Habari mstaafu,
Dk.Harrison Mwakyembe kwamba amefariki dunia.
"Kuanzia Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita kuna taarifa zilizokuwa
zikisambazwa kwanza kwa simu na 'message' za kawaida kuwa nimefariki dunia.
Kesho yake zikaanza kurushwa kwenye TV ya mtandao iitwayo Kalomba TV kwa
kutumia picha zangu mbili tofauti," alisema Dk.Mwakyembe.
Dk. Mwakyembe akizungumza na gazeti hili,
hakukana wala kukubali kulihusisha tukio hilo na njama za kisiasa kwani
lilianza kusambazwa siku ya ziara ya Rais wa Jamhuri wilayani Kyela.
Alisema kuwa taarifa hiyo ya Kalomba TV imesababisha mtafaruku mkubwa
kwenye familia yake ambapo watoto wake na baadhi ya ndugu zake wa karibu
waliumia kisaikolojia na wengine kupata shinikizo la damu.
"Nahisi waliopanga njama hiyo walitaka nipokewe kwenye mkutano wa Rais
kwa nderemo na mhemko mkubwa na pengine hata kuvuruga kwa muda mkutano wa Rais
halafu baadaye nisingiziwe kuwa nilitengeneza mwenyewe taarifa hiyo ya msiba
ili nipokewe na wananchi kwa hisia kali”, alisema.
Aliongeza kuwa kwa bahati chale zikamcheza, akaamua kurudia njiani.
Dk.Mwakyembe ambaye alikuwa waziri katika wizara mbalimbali ikiwemo ya Habari, alishamtaarifu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia,Nape Nauye, kuhusu suala hilo naye akaahidi kulifanyia kazi.
0 comments:
Post a Comment