Na Salma
Haroun
MAKAMU wa
Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt , Philip Mpango ameitaka wizara ya
kilimo kufanya kazi na shirika la Taifa la bima ili kuhakikisha wakulima
hawapati athari zozote katika kilimo dhidi ya madhara yatokanayo na mbegu zisizo
na bora.
Dkt,Philip
Mpango ameyasema hayo Agoust 1jijini mbeya wakati akifungua maonesho ya sikukuu ya Nanenane ambapo amesisitiza
suala hilo waweze kulifanyie kazi ili wakulima kuweza kuepukana na changamoto
katika kupata mbegu zisizo na bora ambazo husababisha wakulima kupata hasara
katika wakati wa mavuno.
Aidha Dkt.
Mpango Amelitaka shirika la utafiti Tari kuwa wabunifu katika kufanya tafiti kwenye mazao mbalimbali
yatakayoweza kutumika katika maeneo tofauti kulingana na ardhi iliyopo hapa nchini.
"Kuna
mbegu zimeenda kwa wakulima wilaya ya
katavi zimeleta balaaa hazikuzaa na wakulima wamesema tari imetudanganya
turekebishe taasisi ya tari ya utafiti ili
kuleta ubora wa mbegu," amesema .
Kwa upande
wake waziri wa kilimo Mh Husseni Bashe, amesema ameziagiza Halmashauri zote wakulima
ambao walitakiwa kulipia mbegu za Ruzuku wasilipie mwaka huu ili kweza kuwapunguzia hasarai
walizo zipata mwaka janaa.
Pia Bashe
amewataka wakulima waweze kuwa na utayari wa kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa
ambapo ni chanzo kimojawapo cha mazao kutokubali katika maeneo yao.
"Wakulima walifundishwa kupanda zao la alizeti wakati wakunyesha mvua na wakati wakulima wamepanda hali ya hewa haikuweza kukubali na kupelekea mazao kuathirika hususani katika nyanda za juu kisini ," amesema.
0 comments:
Post a Comment