Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki S. Shemdoe Leo tarehe 3
Septemba, 2020 ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) ya
Uwezeshaji Biashara katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) jijini
Dodoma.
Lengo
la kikao hiki lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa maelekezo ya mkutano wa
kwanza wa kamati hiyo uliofanyika tarehe 13 Februari 2020.
Masuala
yaliyojadiliwa na kuidhinishwa ni pamoja na hadidu za rejea (ToR) za kamati ya
kitaifa ya uwezeshaji biashara, Maeneo ya kundi A, B na C ya mkataba wa
uwezeshaji biashara wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO TFA) ambayo
yatawasilishwa sekretarieti ya WTO kabla ya tarehe 22 Septemba, 2020.
Utekelezaji wa masuala mengine ya biashara nje ya mkataba wa uwezeshaji biashara, utekelezaji wa mpango mwelekeo (Roadmap) wa miaka mitano (2020/21 - 2024/2025) na mpango kazi (Action Plan) ya mwaka 2020/2021. Aidha, Kamati imetoa maelekezo ya maboresho ya Mfumo wa taarifa za ufanyaji biashara (National Trade Information Module) kabla ya kufanyiwa uzinduzi rasmi.
0 comments:
Post a Comment