![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/1-72-1024x683.jpg)
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mtaa wa
Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua
utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/2-60-1024x683.jpg)
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Ilemela Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa Mtaa wa
Kabangaja kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua
utendaji kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/3-48-1024x683.jpg)
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa na wananchi wa Mtaa wa Kabangaja
kata ya Bugogwa mkoa wa Mwanza wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji
kazi katika sekta ya ardhi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa jana.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/4-33-1024x683.jpg)
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa amemshika Mbuzi kabla ya kukabidhi
kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya MAGA NDONDO CUP ambapo timu ya
Warrious iliibuka mshindi wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya Best
kwa mikwaju ya penati 3-1.
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/5-31-1024x683.jpg)
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo
la Ilemela Dkt Angeline Mabula akiwa amemshika Mbuzi kabla ya kukabidhi
kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya MAGA NDONDO CUP ambapo timu ya
Warrious iliibuka mshindi wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya Best
kwa mikwaju ya penati 3-1.
…………………….
Na Munir Shemweta, WANMM ILEMELA
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amewataka wananchi kuchangamkia zoezi la urasimishaji linaloendelea
nchini ili waweze kuwa na umiliki halali wa ardhi yao watakayoweza
kuitumia kujiletea maendeleo.
Dkt
Mabula ambaye ni Mbunge la Ilemela mkoani Mwanza alitoa kauli hiyo
mwishoni mwa wiki alipozungumza na wananchi wa jimbo lake katika Mtaa wa
Kabanganya kata ya Bugogwa wilaya ya Ilemela mkoa wa Mwanza akiwa
katika ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika
Kanda ya Ziwa.
Alisema,
Rais wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli ameelekeza maeneo yote
yaliyokuwa katika ujenzi holela yarasimishwe kwa kupimwa ili wananchi
wake wawe na umiliki halali kwa kuwa walitumia nguvu nyingi wakati wa
kuyaendeleza.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kupimiwa
pekee katika maeneo yaliyorasimishwa hakutoshi na kushauri wananchi
kuhakikisha wanapata hati za umiliki ili waweze kuzitumia katika
kujipatia mikopo na shughuli nyingine za kimaendeleo.
‘’Wananchi
walijenga kwa nguvu zao, serikali haikuwa makini katika kupanga maeneo
ili watu wakae katika mpangilio mzuri hivyo Rais aliagiza wananchi warasimishiwe
ili waweze kuwezeshwe kiuchumi na kutumia ardhi yao na majengo
kuendelea katika shughuli za uchumi na kuweka dhamana na zoezi hili
linafanyika kwa miaka kumi na kumalizika 2023’’ alisema Dkt Mabula.
Akizungumzia shughuli za maendeleo katika jimbo lake la Ilemela, Dkt Mabula alisema tangu achaguliwe kuwa Mbunge wa jimbo
hilo amefanya mambo makubwa katika sekta ya elimu kwa kuwezesha ujenzi
wa shule za msingi na sekondari sambamba na kuongeza vyumba vya madarasa
kwa baadhi ya shule hizo tofauti na miaka ya nyuma.
Pamoja
na mambo mengine, Dkt Mabula aliwaambia wananchi wa mtaa wa Kabangaja
kata ya Bugogwa mkoani Mwanza kuwa, hivi sasa jitihada inafanyika
kuondoa tatizo la maji katika mtaa wa Kabangaja na mitaa mingine ya
jimbo hilo ambapo tayari timu ya wataalamu iko katika mtaa huo
kuhakikisha inakamilisha uwekaji miundombu ya maji.
Baadhi
ya wananchi wa jimbo la Ilemela katika mtaa wa Kabangaja walimueleza
Dkt Mabula kuwa wanakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji katika maeneo
yao ingawa mtaa wao ndiyo chanzo cha maji kuelekea maeneo mengine.
Mkazi
wa Kabangaja Aziz Said alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi kuwa pamoja na uwepo zoezi la upimaji shirikishi
katika eneo hilo lakini hadi sasa bado hawajapatiwa hati za umiliki wa
maeneo yao jambo lililofafanuliwa na afisa Mipango Miji na Ardhi kutoka
Manispaa ya Ilemela William Magoha kuwa limesababishwa na baadhi ya
wananchi kushindwa kukamilisha fedha za upimaji
0 comments:
Post a Comment