*******************************
Ikiwa Imesalia siku
moja kabla ya kufungwa kwa zoezi la kuandikisha wananchi kwenye Daftari
la kudumu la Wapiga kura kwajili ya Kuchagua viongozi wa ngazi ya Mtaa,
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa kutambua umuhimu wa
zoezi hilo amewaelekeza wenye maduka kufungua maduka yao Kesho October
14 kuanzia saa tano ili kutoa nafasi kwa wananchi kwenda kujiandikisha.
RC Makonda amesema
kwakuwa kesho ni Siku ya Kumbukumbu ya Miaka 20 ya kifo cha Baba wa
Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameona ni vyema Wananchi wote
wakamuenzi Baba wa Taifa kwa kuhakikisha wanapata Nafasi ya Kutosha ya
Kujiandikisha ili waweze kuchagua Viongozi wa mitaa wanaoweza kutatua
matatizo yao.
Aidha RC Makonda
amewasihi Wamachinga, Bodaboda, Makondakta, madereva, Viongozi wa
Taasisi, wafanyakazi wa Bar, Saloon, wamiliki na wafanyakazi wa Sehemu
za Starehe kuhakikisha wanajiandikisha kwenye Ofisi za Serikali ya Mtaa,
Shule za Msingi, sekondari na sehemu zilizowekwa mahema maalumu ya
kujiandikisha.
EWE MWANANCHI TUMIA HAKI YAKO YA MSINGI YA KUJIANDIKISHA KWAAJILI YA KUCHAGUA VIONGOZI WENYE SIFA.
0 comments:
Post a Comment