![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-NO.-1.jpg)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati, kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Afisa Madini
Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo wakielekea eneo lenye mgogoro
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/AA-4.jpg)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akisikiliza kero za
wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu katika eneo la Misigiri Wilayani
Iramba Mkoa wa Singida
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-NO.-3.jpg)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo kushoto akiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula wakijadiri jambo baada ya
kuwasili kwenye eneo lenye mgogoro katika Kata ya Misigiri Wilayani
Ilamba Mkoa wa Singida
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-NO.-4.jpg)
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula kulia akimuelekeza Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo eneo lenye mgogoro
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-NO.5.jpg)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikakati, kushoto
ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Afisa Madini
Mkazi wa Mkoa wa Singida Chone Malembo wakijadiri jambo wakati
wanaelekea eneo lenye mgogoro
![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2019/10/PICHA-NO-6.jpg)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo katikati, kushoto ni
Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Immanuel Luhahula, Kulia ni Nabii Elia ambaye
ndiye anae chimba eneo hilo lenye mgogoro
……………………
Serikali imeingilia kati mgogoro uliodumu kwa muda mrefu
katika eneo la wachimbaji wadogo lililopo katika Mlima wa Sakenke kata
ya Misigiri Wilaya ya Iranga Mkoani Singida.
Mgogoro huo uliodumu kwa takribani miaka 3 ni kati ya
mchimbaji mdogo aliyekuwa afisa usalama wa taifa mstaafu John Lutebeka,
na Nabii Elia wote wanagombea eneo hilo ambalo Lutebeka anamiliki ardhi
ya juu na Elia ameliombea Leseni ya Uchimbaji Madini.
Akizungumza kwenye eneo linalogombewa, Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo, amewataka Lutebeka, Nabii Elia na Afisa Madini
Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo wafike ofisini kwake Jijini
Dodoma siku ya Jumatano Oktoba 16 mwaka huu kwa ajili ya kutatua mgogoro
huo na kila mmoja aje na vielelezo vinavyomruhusu kuchimba madini
katika eneo hilo.
Aidha, Nyongo amewataka Maafisa Madini kote Nchini kutoa
elimu kwa wachimbaji juu ya sheria za madini ili kuepusha migogoro isiyo
ya lazima maana kuna haki ya umiliki wa ardhi ya juu na kuna haki ya
umiliki wa ardhi ya chini kwa maana ya leseni ya uchimbaji hawa wote
wana haki sawa wanaweza wakakaa wakazungumza wakachimba pamoja.
Wakati huo huo Naibu Waziri Nyongo, amemtaka Nabii Elia
aachane na uchimbaji wa madini karibu na nguzo za umeme anatakiwa awe
mita 100 kutoka kwenye nguzo za umeme, vinginevyo atachukuliwa hatua.
Pia nyongo amewapongeza wachimbaji wa madini wa Mkoa wa
Singida kwa ulipaji mzuri wa kodi na amesema rasilimali ya madini ni ya
Watanzania wote, hatuko tayari kumuoneo mtu wala hatakubari mtu achimbe
amdhulumu mwingine.
“Kwenye uchimbaji kuna kelele nyingi, kuna wengine wanamiliki
leseni nyingi hata kuzihudumia hawawezi, mpaka sasa tumefuta leseni
elfu 13 hivyo wale wanaojua wasitumie ujuaji wao kuwadhuru wengine
tutampa haki mwenye haki yake,” alisema Nyongo.
Awali Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Malembo, alisema
kwa nyakati tofauti, ofisi yake imesuluhisha mgogoro huo, lakini
Lutebeka huwa haridhiki na maamuzi tunayofikia ikabidi tuligawe eneo
hilo leye hekari 7.2 na kumpa Lutebeka hekari 4 lakini bado hakuridhika.
Akizungumza kwa masikitiko, Mkuu wa Wilaya ya Iramba
Huhahuka amesema anasikitika kuingizwa kwenye mgogoro huo ambapo Afisa
Usalama wa Taifa Mstaafu Lutebeka amekuwa akimtuhumu kuwa anawadhamini
hao wanaotaka kuchimba eneo hilo.
Kwa mujibu wa Afisa Madini Mkazi wa Singida, Malembo amesema,
kati ya Julai na Oktoba 11 mwaka huu, wamekusanya mapato ya zaidi ya
shilingi 1.3 bilioni, Mapato hayo ni sawa na asilimia 271.94 ya lengo
kwa awamu ya kwanza la kukusanya shilingi 500,000,000, na asilimia 90.65
ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi 1,500, 000,000/=.
0 comments:
Post a Comment