METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, August 21, 2020

HASUNGA ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE CCM JIMBO LA VWAWA

Waziri Japhet Hasunga akionyesha fomu ya kugombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi mara baada ya kukabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Mbozi Bi Hanji Godigodi leo Tarehe 21 Agosti 2020.

Waziri Japhet Hasunga akikabidhiwa fomu ya kugombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Mbozi Bi Hanji Godigodi leo Tarehe 21 Agosti 2020.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 2020-2025.

Waziri Hasunga amekabidhiwa fomu hiyo leo Tarehe 21 Agosti 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Mbozi Bi Hanji Godigodi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com