NA. MWANDISHI WETU
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Yaridhishwa na
hatua iliyofikiwa katika kuwawezesha vijana takribani 3440 kukuza ujuzi wao
kupitia programu ya Ukuzaji ujuzi inayotekelezwa na Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu .
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Nagma Giga amesema kuwa mradi huo ni muhimu
katika kuiwezesha nguvu kazi ya Taifa hasa vijana kuwa na ujuzi stahiki.
“Tunaipongeza Serikali kwa mkakati huu utakaowezesha kupanua wigo
wa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika nchi yetu”alisema Giga.
Mradi wa mafunzo ya ufundi stadi kwa Vijana unatekelezwa kupitia chuo
cha ufundi stadi DONBOSCO kwa ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
ambapo katika mwaka wa fedha 2019/2020 vijana elfu 10,000 wanatarajiwa
kunufaika na mpango huo.
Akizungumza wakati wa ziara ya Wabunge hao mwishoni mwa wiki Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Antony
Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya
Taifa inakuwa na ujuzi unaoendana na mahitaji ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
Aliongeza kuwa kuwajengea uwezo Vijana kwa kuwapa ujuzi stahiki
kunawawezesha kujiajiri na kuzalisha ajira hali inayowawezesha kuchangia katika
kukuza uchumi na kuchangia maendeleo ya Taifa.
Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye
Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Vijana wanayo nafasi kubwa ya
kuchangia katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia ujuzi wanaopata kupitia
programu hiyo.
"Pamoja na changamoto ya ajira kwa vijana, Serikali yetu sikivu
imeendelea kuwapa kipaumbele vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili
ikiwemo suala la ukosefu wa ajira kupitia utekelezaji wa programu hii itawezesha
vijana wengi kujiajiri na kuchangia kukuza uchumi"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally
Msaki amesema kuwa uwezeshaji Vijana umepewa kipaumbele kupitia programu hiyo
na utaratibu huo ni endelevu kwa dhamira yakuwafanya vijana wachangie katika
kukuza uzalishaji na tija.
Wakizungumza wakati wa ziara ya Kamati hiyo Katika Chuo cha Ufundi Stadi
DONBOSCO cha Jijini Dodoma baadhi ya wanufaika akiwemo Bi. Esther Ngallya
amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuwawezesha Vijana kujikwamua
kiuchumi kupitia programu ya kukuza ujuzi inayotekelezwa kupitia chuo hicho.
Akiafafanua amesema kuwa Serikali imebadili mwelekeo wa maisha ya Vijana
walionufaika na Programu hiyo ambao wanauwezo mkubwa kwa sasa nyanja za umeme,
ujenzi, tarazo,useremala, umeme, ufundi bomba na nyingine nyingi.
Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuwawezesha Vijana kupitia
programu mbalimbali ikiwemo ya kukuza ujuzi na ile ya ujenzi wa vitalu nyumba
katika kila Halmashauri ambapo vijana 100 katika kila halmashauri wanajengewa
uwezo ili waweze kutekeleza azma ya kuchangia katika kukuza uchumi na ujenzi wa
viwanda.
=MWISHO=
0 comments:
Post a Comment