Na
Issa Mtuwa- Morogoro
Mwenyekiti
wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amekerwa na kukasirishwa na ukosefu wa
uadilifu kwa wafanyakazi wa Tume ya Madini katika baadhi ya Ofisi na kueleza
kuwa, suala hilo halitavumilika kwa wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Tume ya Madini Mkoa wa Morogoro katika siku ya kwanza ya
ziara yake aliyoianza Aprili 8, 2019, Prof. Kikula amewaeleza wafanyakazi wa
ofisi hiyo kuwa, yeye na viongozi wenzake wa tume wamekerwa na kusononeshwa na
vitendo vya ukosefu wa uadilifu vinavyofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya
Madini.
Ametolea
mfano wa kitendo kilichofanywa na wanafanyakazi wa Tume hiyo wilayani Chunya ambapo
watumishi wote wa kituo hicho wamesimamishwa kazi na Waziri wa Madini Doto
Biteko kutokana na kukosa uadilifu na kutoa taarifa isiyo sahihi kwenye takwimu
za madini.
“Kuna
udanganyifu mkubwa unaofanywa na wachenjuaji madini, na udanganyifu huo unachochewa
na watumishi wa Tume. Angalia mfano pale Chunya, wale wachenjuaji wamedanganya
lakini ukifuatilia utagundua wafanyakazi wa tume wanahusika na huo udanganyifu,
na ndio maana hata Waziri wa Madini aliamua kuchukua hatua ya kuwasimamisha
kazi wafanyakazi wote wa kituo kile,” amesema Prof. Kikula.
Kufuatia
hali hiyo, Prof. amekemea vitendo hivyo na kueleza kuwa, suala la uadilifu ni
muhimu katika kazi za watumishi wa tume na kueleza kuwa, pamoja na kuwepo vishawishi
vingi katika sekta ya madini, lakini wanapaswa kukumbuka kuwa kazi ni muhimu
kwao na familia zao.
“Mimi
na wenzangu tunaumizwa moyoni tunapoona wafanyakazi wa Tume wanakutwa na hatia ya
ukosefu wa uadilifu inatusikitisha sana, sana”, amesisitiza Prof. Kikula.
Akitolea
ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yaliyowasilishwa na Kaimu Afisa Madini
Mkazi, Prof. Kikula amewapongeza watumishi
wote wa kituo cha madini Morogoro kwa
kazi nzuri ya kusimamia ukusanyaji wa maduhuli na kuwaomba kuongeza bidii ili
wafikie malengo waliyojiwekea.
Kuhusu
masuala ya leseni, Prof. Kikula amemuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi kufuatilia
leseni zote zilizopo na kubainisha leseni ambazo sio hai na kuzifuta kwa mujibu
wa sheria. Aidha, amekumbusha kuhusu kufuata utaratibu halali uliowekwa kwa
mujibu wa sheria katika hatua za ufutaji wa leseni hizo na kusema “asimuogope
mtu lakini pia asimuonee mtu katika hatua hiyo ya ufutaji wa lesini zisizo hai”.
Aidha,
Prof. Kikula amekiri kuwepo kwa changamoto na kuwataka watumishi hao kuwa na
subira na kuongeza kuwa, Tume imepanga kununua magari 34 ambayo yatasambazwa
katika mikoa yote ili kuongeza tija. Prof. Kikula amezungumza hayo baada ya
kuwasilishwa kwa taarifa ya ofisi hiyo ambayo ilieleza kuwepo kwa changamoto
kadhaa.
Kwa
upande wake, Kaimu Afisa Madini Mkazi Morogoro Mhandisi Emmanuel Shija akisoma
taarifa ya ofisi hiyo, pamoja na mambo mengine, amemweleza Mwenyekiti wa Tume masuala
kadhaa yanayosimamiwa na ofisi hiyo ikiwemo uanzishwaji wa soko la Madini, ufutaji
wa lesseni za uchimbaji kwa wamiliki wanaoshindwa kutimiza vigezo vya leseni
zao, ukusanyaji wa maduhuli na changa moto zinazo wakabili katika kutekeleza
majukumu yao.
Mhandisi
Shija amesema, pamoja na changamoto zilipo, ofisi hiyo inafanya jitihada za kusimamia
ukusanyaji wa maduhuli ambapo mpaka sasa imefikia asilimia 53 ya lengo na kwamba,
inategemea kufikia malengo ya ukusanyaji waliyojiwekea.
Naye,
Kamishna wa Tume ya Madini Dkt. Athanas Macheyeki ambaye amembatana na Mwenyekiti wa Tume, amewapongeza
kwa ukusanyaji mzuri wa maduhuli na
kuwataka kujiwekea muda wa utekelezaji wa malengo ili waweze kujipima vizuri.
“Unapojiwekea
muda wa utekelezaji unakufanya uongeze bidii pindi unapoona uko nyuma ya muda
ya utekelezaji wa lengo hivyo ni muhimu wa kulizingatia hilo,”amesema Dkt.
Macheyeki.
Prof.
Kikula na Dkt. Macheyeki wako mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi kukagua
utekelezaji wa shuguli za Tume katika Wilaya mbalimbali zinazofanya shuguli za
madini sambamba na kutatua kero za wachimbaji na wadau wa madini, mkoani humo.
0 comments:
Post a Comment