Pichani Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mheshimiwa Kenani Kihongosi
akizungumza na wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mkuu BAKWATA mkoa wa Arusha.Picha
na Innocent Natai
Pichani Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Mheshimiwa Kenani Kihongosi pamoja na viongozi wa Baraza la waislam
Tanzania(BAKWATA) Mkoa wa Arusha na Taifa
Na Innocent Natai, WazoHuru- Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe Kenani Kihongosi amewataka viongozi wa Dini Mkoa wa Arusha kudumisha ushirikiano baina yao na serikali,ili kuondoa kero mbalimbali na kusaidiana na serikali kuhamasisha maendeleo katika MKOA wa Arusha na na nchini kwa Ujumla,ameyasema hayo mapema hii leo akifungua mkutano wa uchaguzi baraza kuu la waislam BAKWATA mkoa wa Arusha katika ofisi za Baraza hilo Arusha.
Kihongosi
amesema viongozi wa dini wanamchango mkubwa katika Taifa hasa katika kuwashauri
viongozi na kuliombea Taifa na ndio maana kiongozi mkuu wa nchi aliweka imani
kubwa kwao na kufanya kitendo cha kishujaa kwa kutangaza siku tatu za
maomnbi na kuwataka waliombee taifa dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona
kitendo kilicho ipa ushindi taifa letu ushindi dhidi ya maambukizi hayo.
Ameongeza
kuwa kitendo hicho kiliyashangaza mataifa makubwa kwa kuliona taifa letu lenye
kiongozi shupavu linaepukana na vifo vya virusi vya Corona, huku katika mataifa
hayo maambukizi na vifo vya wagonjwa wa Corona yakiongezeka kwa kasi.
Amesema
kwenye nchi yetu hayo hayakutokea kwa sababu tuna kiongozi makini mwenye hofu
ya Mungu na kiongozi anaeshirikiana kikamilifu na viongozi wa dini bila kubagua
dini,tunamshukuru kwa kuona kuna umuhimu wa kumtanguliza mwenyenzi Mungu na
viongozi wa dini katika majanga yote yanayolikumba taifa letu.
Ameongezakuwa
nchi ya Tanzania tuna bahati ya kumpata Rais na viongozi wakuu wa Serikali
wanaopenda mashirikiano na viongozi wa dini,kwahiyo umoja na ushirikiano baina
ya viongozi wa Serikali na dini udumishwe na tusikubali awepo wa kuuvunja
ushirikiano huu ili uweze kuleta maendeleo na amani katika nchi yetu.
“Kupitia
janga la virusi vya Corona Mwenyenzi MUNGU ametuonyesha ni kwanamnagani
Tanzania tuna RAIS bora baada ya mataifa mengine kuamua raia wao wafungiwe yeye
aliwataka watanzania wamwombe Mungu na wafanye kazi,tunaweza kusema Tanzania
tuna *extra ordinary President* ambae yeye anamaono ambayo viongozi wengine
hawakuwanayo Dunia nzima”aliongeza Dc Kenani
Aidha
amewataka viongozi watakao chaguliwa wahakikishe wanawaunganisha waumini wao na
kuwahamasisha kufanya kazi kwa bidii ili kulikomboa Taifa na uchumi wa
familia kama ilivyo adhima ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na
Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli inayolenga kuhakikisha kipato cha Mtanzania
kinaongezeka.
Katika
mkutano huo wa Uchaguzi Mhe Kenani Kihongosi alimwakilisha Mkuu wa mkoa wa
Arusha MH.IDD HASSAN KIMANTA ambapo uchaguzi huo ulilenga kupata wajumbe
watakao wakilisha baraza hilo(BAKWATA) kimkoa katika uchaguzi mkuu wa
BAKWATA kitaifa.
Mkutano
huo Ulihudhuliwa na KATIBU MKUU WA BAKWATA TANZANIA ,pia ulijumuisha wajumbe 50
kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha ikiwemo mashehe,makatibu,wenyeviti wa
baraza hilo halmashauri ya mkoa,mhasibu,jumuiya ya wanawake na viongozi wa juu
wa Mkoa pamoja na wajumbe wa kualikwa.
Hongra saana Mhe.Kenani DC Arusha.
ReplyDeleteMungu akuongoze ndugu KENANI
ReplyDeleteHongera DC mpya chapa kazi tuulinde Uhuru wetu
ReplyDelete