Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.
Mhandisi Stella Manyanya amekabidhi malighafi (Ethanol) inayotumika kutengeneza
vitakasa mikono ( Hand Sanitizer) iliyotolewa na kiwanda cha Kilombelo Sugar
Company Limited na Wizara kuchukua jukumu la kugawa malighafi hiyo kwa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi ya utafiti wa
Teknolojia (TIRDO) pamoja na taasisi ya kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO).
Hii imekuja kutokana na kikao cha Tarehe 25
Machi, 2020 kilichoitishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent
Bashungwa alipokutana na wenye Viwanda vya kuzalisha malighafi zinazotumika
kutengeza vitakasa mikono (Hand sanitizer). Kampuni ya Consumer choice kwa
kuona umuhimu wa agizo la waziri la viwanda hivi kusaidia kusaidia mapambano
dhidi ya ugonjwa huu wa Korona (COVID 19) Kiwanda hiki kilibeba jukumu la
kusafirisha ethanol lita 30,000 zilizotolewa na Kilombero Sugar Company Limited
kuzileta Dar es salaam ili kukabidhi kwa Wizara ya Afya, TIRDO na SIDO.
Pamoja na ahadi hiyo Kampuni ya Consumer Choice
iliamua kubadili 75% ya ethanol iliyokuwa ikitumika kutengeza kilevi itumike
kutengeza vitakasa mikono (Hand sanitizer).
Kampuni ya Consumer
Choice kwa kushirikiana na kampuni ya G & Co. Limited & Sanitation
Ltd na kufanikiwa kutengeneza vitakasa mikono (Hand sanitizer) Lita 11,000
zilizotokana na lita 8,000 za ethanol kati ya lita 20,000 walizopewa wizara ya
afya.
Naibu Waziri Mhandisi Stella Manyanya
ameishukuru Kampuni ya Consumer Choice
kwa kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na ugonjwa wa COVID 19 kwa
kuunga mkono mchango wa Kilombero Sugar kwa kugharamia gharama za
usafirishaji wa malighafi hii ya ethanol kutoka kiwandani Kilombero hadi
Dar es salaam.
Mhe. Manyanya amesema kuwa “Wizara ya Viwanda
na Biashara kwa kushirikina na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto kufanya kazi usiku na mchana kupambana na janga
hili kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa kinga vya kuzuia usambaaji wa ugonjwa
huu vinapatikana kwa wingi”.
Mhe Manyanya ametoa wito kwa wenye viwanda vya
kutengeneza vifaa kinga nchini kuongeza bidii katika uzalishaji ili kuwezesha
maeneo yote ya nchi kupata vifaa hivyo kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Ameongeza kwa kusema
kuwa taasisi
zinazopokea malighafi kutumia malighafi hiyo kuokoa maisha ya watanzania kwa
kuzalisha vitakasa mikono vyenye bei nafuu.
Aidha Mhe. Manyanya amewasihi wadau wengine
wenye viwanda vyenye mifumo inayoweza kutengeneza vitakasa mikono kuweka nguvu
kwenye uzalishaji wa vifaa hivi kwa wingi ili kusaidia mapambano haya.
0 comments:
Post a Comment