Na. Tito Mselem, Morogoro,
Waziri
wa Madini Dkt. Doto Biteko amewataka wachimbaji wa madini wa vijiji vya Lubungo
Kata ya Mikese na Maseyu Kata ya Dwata wilaya ya Morogoro kuachana na migogoro
katika maeneo yao ya uchimbaji na badala yake washirikiane katika shughuli zao
cha uchimbaji madini.
Dkt.
Biteko ametoa kauli hiyo alipotembelea vijiji hivyo vyenye shughuli za
uchimbaji madini ya dhahabu ambapo amesema migogoro baina ya wawekezaji wa
madini na wachimbaji wadogo mkoani Morogoro inatakiwa kuisha kwa wao wenyewe
kushirikiana kwa kufuata Sheria na Kanuni zilizopo na kueleza kuwa migogoro
hiyo hailipi na badala yake inazidi kuwarudisha nyuma na kukimbiza maendeleo
kwenye maeneo yao.
Aidha,
Dkt. Biteko amesema mapinduzi katika Sekta ya Madini yameongezeka katika
kipindi cha uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu
Hassan ambapo mapato yatokanayo na madini kuongezeka.
Sambamba
na hayo, Dkt. Biteko amesema kwa sasa wawekezaji kutoka nje wanakuja kwa wingi
kutokana na kufunguliwa kwa milango ya nchi ambapo hivi karibuni inchi
ilishuhudiwa kusainiwa kwa mikataba mikubwa ya uchimbaji madini.
Pia,
Dkt. Biteko amewataka wachimbaji wa madini nchini wanamuunge mkono Rais Samia
Suluhu Hassan kutokana na namna alivyoweza kufanya ushawishi wa kuwaleta
wawekezaji baada ya kwenda nje ya nchi na kufanya mazungumzo na viongozi
wenzake.
“Mimi
na wenzangu kutoka Wizara ya Madini tunaona, juzu juzi tumesaini mikataba mingi
ya uchimbaji mkubwa wa madini ambayo hatujawahi kutokea ila katika kipindi cha
Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan imetokea,”amesema Dkt. Biteko.
Pamoja
na mambo mengine, Dkt. Biteko amesema kwa sasa Serikali inafanya juhudi za
makusudi kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika uchumi wa madini
na kuzifungamadisha sekta zingine katika fursa zilizopo kwenye sekta hiyo.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando amempongeza Dkt. Biteko
kwa kutembelea wilaya hiyo na kumuahidi kuyafanyia kazi maagizo yake yote
atakayo yatoa.
Msani amesema uongozi wa wilaya yake utasimamia Sekta ya Madini kikamilifu pamoja na kutatua kero zitokanazo na sekta hiyo sanjari na kuboresha maisha ya wananchi wa eneo hilo ambao licha ya madini kuwepo katika maeneo yao lakini bado wanaishi katika nyumba za matope na majani.
0 comments:
Post a Comment